Mwakalebela:Nitajenga viwanja vipya mikoani - KULUNZI FIKRA

Wednesday, 9 August 2017

Mwakalebela:Nitajenga viwanja vipya mikoani

Mgombea wa nafasi ya urais katika Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania Frederick Mwakalebela kwamba endapo atachaguliwa kuwa Rais wa TFF,basi atahakikisha anajenga viwanja vipya vya kisasa katika mikoa karibu yote.
Mwakalebela aliyasema hayo leo alipokua anazindua kampeni zake za kuwania Urais katika ukumbi wa Hotel ya Double View iliyopo Sinza Mapambano.

Mwakalebela amesema alipokua Katibu mkuu wa TFF alianzisha mchakato huo na alipata eneo la kujenga uwanja Kule mkoani Tanga katika eneo la Mnyanjani lakini kwa bahati mbaya alipoondoka katika nafasi hiyo uwanja ule haukujengwa na waliomfatia, na sasa anaomba ridhaa ili pamoja na mambo mengine aendeleze pale alipoachia katika kujenga viwanja vipya vya mpira wa miguu Tanzania.
Mwakalebela alitolea mfano wa Mkoa wa Pwani ambao hauna kabisa uwanja wenye hadhi wa kuchezea ligi kuu ya Tanzania Bara.

Mwakalebela alisema kwamba ujenzi wa viwanja hivyo utasaidia katika kuinua kiwango cha mpira wa miguu Tanzania na kuibua vipaji vipya na hamasa kwa Vijana katika kucheza mpira wa miguu jambo litakalosaidia Taifa siku za mbeleni kwenye timu ya Taifa Stars.
Mwakalebela anaingia katika ushindani wa nafasi ya Urais wa TFF huku akiwa analindwa na historia nzuri ya uadilifu, uaminifu na uchapakazi uliotukaka katika kuiwezesha Taifa Stars Kushiriki michuano ya CHAN mwaka 2009, kuiwezesha timu ya wanawake Twiga Stars kushiriki michuano ya AFCON kule nchini South Africa,kuleta maendeleo ya soka kwa kuongeza udhamini na wadhamini katika mpira wa miguu Tanzania, kuufanya mpira wa miguu kama biashara na ajira rasmi kwa wachezaji ,kuanzisha ligi za Vijana kama Copa Coca cola, Airtel Raisingi Star na Uhai Cup michuano iliyosaidia kuibua nyota wengi kama akina Thomas Ulimwengu na Mbwana Samatta.

No comments:

Post a Comment

Popular