Mpinzani mkuu wa Lungu atoka jela - KULUNZI FIKRA

Wednesday, 16 August 2017

Mpinzani mkuu wa Lungu atoka jela

Kiongozi mkuu wa upinzani nchini Zambia, Hakainde Hichilema Aliyekuwa amewekwa mahabusu akikabiliwa na shtaka la uhaini ameachiwa Uhuru asubuhi ya leo .
Hichilema ameachiwa Uhuru baada ya mwendesha mashtaka kufutiwa mashtaka kiongozi huyo aliyekuwa mahabusu yangu Aprili mwaka huu.
"Mwendesha mashtaka ameamua kusitisha mchakato wa kesi mamlaka ya kikatiba aliyonayo.kwa hiyo,ameachiwa huru kuanzia sasa ", amesema maji was mahakama kuu , Charles Chanda.
Hichilema na wenzake walikamatwa kwa madai ya kutaka kuatarisha maisha ya Rais Edga Lungu baada ya kiongozi huyo na wafuasi wake kukataa kupisha msafara wa Rais huyo.
Habari za kuachiwa huru zilivuja toka mwishoni mwa wiki, ukielezwa kwamba ni kutokana na na juhudi zilizo fanywa na katibu mkuu wa jumuiya ya madora Patricia Scotland ambaye alifanya ziara nchini Zambia kuangalia halia ya siasa,katibu huyo alikutana na mazungumzo na Rais Lungu na pia alimtembelea Hichilema katika gereza la mukabeko.

No comments:

Post a Comment

Popular