Mkuu wa wilaya Hai, amuweka mwalimu rumande kwa kushindwa kujibu swali - KULUNZI FIKRA

Sunday, 20 August 2017

Mkuu wa wilaya Hai, amuweka mwalimu rumande kwa kushindwa kujibu swali

 
 Katika ziara ya kutembelea shule za sekondari,Mkuu wa wilaya ya Hai,Mh.Gelasius Byakanwa alifika shule moja iliyopo ukanda wa chini mwa wilaya ya hiyo akiambatana na afisa elimu msaidizi ndugu Jafari na mwandishi wa habari wa Redio Boma-Hai FM ndugu Davis Minja.

Dc alifanya kikao na walimu hao,alianza kwa kuwauliza wangapi wanamfahamu kwa majina,walimu walikaa kimya,dc akawaamuru waandike majina yake kwenye karatasi aliyowapa.Baadhi ya walimu walishindwa na kuwaita WANAFIKI.kosa ni kushindwa kuandika majina yake.
Baada ya muda akawataka waalimu waandike nafasi ya shule mwaka 2015 katika mtihani wa taifa ( NECTA) ,mwalimu mmoja alishindwa kuandika na alipomfata akimwamuru aandike,mwalimu alimjibu hawezi kuandika uongo kwani hakumbiki.Jibu hilo lilimfanya DC apige simu Polisi na kuagiza polisi waje.

Kabla gari la polisi kuja,DC alimwita mwalimu pembeni na kumwambia achague kati ya kwenda rumande au kupiga push-up 20,lakini mwalimu alimjibu hawezi kupiga push-up kwani anamatatizo ya kiafya.Basi gari lilipokuja mwalimu alipandishwa na kupelekwa kituo cha polisi Bomang'ombe.

Dc aliwaambia walimu wakitaka wakashitaki kokote na hata kwenye  chama chao cha CWT.
Kisha aliwaamuru kupiga picha ya pamoja kama kumbukumbu.
 Dc amekuwa akiwapigia simu walimu hao na kutaka kujua kinachoendelea.

Taarifa ilifikishwa chama cha waalimu CWT-wilaya na kisha kuja kufanya kikao na waalimu ilikupata uhalisia wa tukio,ndio mwalimu mmoja wa kike kuongeza kuwa baada ya kikao kwisha DC alimpigia simu saa zisizo za kazi ikiwa ni pamoja na usiku akimtaka waonane.Mwalimu alitoa vielelezo vya sms na muda aliopigiwa (screen shoot) zake na kumkabidhi katibu wa CWT mkoa wa kilimanjaro.

No comments:

Post a Comment

Popular