Akihutubia mkutano wa umma katika wadi ya Murieti, Lema alimsifu Rais Kenyatta na kusema ameoonyesha ukomavu wa kisiasa kwa kuwaruhusu wapinzani wanaomtuhumu kwamba alihusika na udanganyifu katika uchaguzi mkuu uliokamilika hivi majuzi kufanya maandamano mbali na kuwapatia maafisa wa usalama kuwalinda
Kulingana na gazeti hilo, Rais Uhuru Kenyatta ambaye alikuwa akitetea kiti chake aliibuka mshindi katika uchaguzi huo kwa kupata asilimia 54 ya kura huku mpinkumuiga zani wake Raila Odinga akijipatia asilimia 44.
Kulingana na Lema maandamano ya upinzani pamoja na mikutano ya uma itaisaidia serikali kwa sababu chama tawala kitaelewa maswala yanayowakabili raia na kuyafanyia kazi huku upinzani ukitekeleza haki yao ya kidemokrasia kupitia kushirikiana na umma mbali na kutatua maswala muhimu yanayowakabili raia.
''Demokrasi ni swala tata, mara nyengine linaweza kuathiri uchumi. Wawekezaji wengi huchunguza kiwango cha demokrasia katika taifa kabla ya kuwekeza. Iwapo tutaendelea na mkondo huu basi utatukwaza katika siku za usoni'', alisema.

No comments:
Post a Comment