Magufuli ateua maprofesa watatu kuongoza taasisi - KULUNZI FIKRA

Friday, 18 August 2017

Magufuli ateua maprofesa watatu kuongoza taasisi

Rais John Magufuli leo ijumaa amefanya uteuzi wa viongozi watatu katika nafasi mbalimbali.
Taarifa iliyotolewa imeeleza kuwa Rais Magufuli amemteua profesa Abdulkarim Mruma kwa mwenyekiti wa kampuni ya kuifadhi mafuta (Tiper) .
Profesa Mruma pia ni mtendaji mkuu wa wakala jiolojia.
Pia Rais Magufuli amemteua profesa Joseph Buchweshaija kuwa mwenyekiti wa kampuni ya puma Energy Tanzania.
Profesa Buchweshaija ni Naibu mkuu wa chuo kikuu kishiriki cha Elimu Dar es salaam (DUCE).
Vile vile Rais Magufuli amemteua profesa Evaristo Liwa kuwa makamu wa chuo cha ardhi (ardhi university).
Profesa Liwa amechukua nafasi ya Idrissa Msharo ambaye amestaafu.Uteuzi wa viongozi hao umeanza Agosti 17,2017

No comments:

Post a Comment

Popular