Luizio: Wala sina presha - KULUNZI FIKRA

Thursday, 31 August 2017

Luizio: Wala sina presha

Dar es Salaam. Mshambuliaji wa  Simba, Juma Liuzio amefichua kwamba hana presha kabisa katika kikosi hicho na ndiyo maana ametulia na kuanza vizuri msimu.

Liuzio ambaye aliifungia Simba bao moja katika ushindi wa mabao 7-0 dhidi ya Ruvu Shooting wikiendi iliyopita, alisema anafurahi kuanza vizuri msimu na anatazama mbele kufanya makubwa.

"Mashabiki wengi hawana matarajio makubwa kwangu, hii inanisaidia kutuliza akili na kufanya vizuri tofauti na wengine," alisema Liuzio.

Akizungumzia upande wa washambuliaji, Liuzio alisema wako vizuri kwa sasa lakini wanahitaji muda zaidi kuweza kutisha zaidi.

"Bado tuna changamoto ya kufanya vizuri, wachezaji wengi ni wapya na wanajipanga kuisaidia timu, kocha bado ana kazi ya kutuunganisha," alisema.

No comments:

Post a Comment

Popular