Kumekuwa na baadhi ya watu wamekuwa wakitushangaa CHADEMA ambacho ni chama kikuu cha upinzani Tanzania kumuunga mkono Rais Uhuru Kenyatta badala ya mpinzani mwenzetu Mh Raila Amolo Odinga. Ukweli ni huu;
■Uchaguzi mkuu wa Kenya uliopita tulimuunga mkono Odinga kwa kuwa hatukumjua vizuri Kenyatta hivyo we stand na Odinga na hata tulipeleka makamanda na vifaa vyetu kusaidiana nae. Dhamira ilikuwa kukuza demokrasia ktk Afrika ya Mashariki.
■Mwaka huu tumemuunga mkono Kenyatta kwa kuwa kila tulichokuwa tunakipigania na kukiamini (DEMOKRASIA NA MAENDELEO) mh Kenyatta ametimiza wajibu huo vyema kuliko kiongozi yeyote ktk ukanda huu wa Afrika Mashariki. Kenya miongoni mwetu imekuwa nchi ya mfano. Utawala bora, uhuru wa wapinzani kukosoa serikali, haki ya wapinzani kufanya mikutano na maandamano kama ilivyoainishwa ktk katiba yao, uwazi ktk utekelezaji wa kazi za serikali na mengi mengine. Lakini pia kuelekea uchaguzi aliunda tume huru ya uchaguzi, mahitaji muhimu ya wapinzani yalisikilizwa (mfano kura kwa wafungwa na walio nje ya nchi) na pia kupitia hotuba zake nyingi alionyesha UPENDO WA WAZI KWA WAPINZANI WAKE jambo ambalo ni adimu na ajabu ktk nchi zetu. Huku kwetu mpinzani kwake jela, mpinzani wake polisi, mpinzani sebuleni kwake mahakamani.
■Ikumbukwe hata hapa Tanzania kuna wapinzani wenzetu na tunawapinga matendo yao yanayoua demokrasia mfano ni Lipumba, Mrema, Cheyo, Zitto na wengine wa aina yao
Lakini kuna wanaccm tunaowaunga mkono katika mengi mfano Hussein Mohammed Bashe marehemu Deo Fulikunjombe, makamu wa rais Samia na wengine wa kaliba hiyo. Hata mh Kenyatta akibadilika kuwa kama madikteta wengine tuwajuao tutapaza sauti kumpinga. Huwezi kuwa na amani wakati kwa jirani hakuko sawa. HATUPELEKWI NA UPEPO TUNAPELEKWA NA MOVIE.

No comments:
Post a Comment