Bavicha walitaka jeshi la polisi kumkamata Ngeleja na kumuacha Tundu Lissu - KULUNZI FIKRA

Thursday 24 August 2017

Bavicha walitaka jeshi la polisi kumkamata Ngeleja na kumuacha Tundu Lissu

 
 Serikali imeshindwa kuongoza nchi kwa kujibu hoja na kufuata sheria.

- BAVICHA inataka kuongelea kuhusu upotevu wa zaidi ya Bil 87 inayotokana na uvunjaji wa mkataba wa Mkandarasi aliyetakiwa kujenga Barabara ya kutoka Wazo mpaka Bagamoyo ulioingiwa 2004 na kuvunjwa na Waziri wa wakati huo(Rais wa sasa).

- Matendo haya yanagharimu Taifa na sisi kama Vijana tunalinda rasilimali zetu na kama wapinzani ni kazi yetu kuonya serikali.

- Chama mnamo Ijumaa Agosti 21, kupitia Lissu kilitoa tamko la kutaka serikali ieleze kuhusu kushikiliwa kwa Bombardier Q400 kwa sababu ya deni hilo.

- Kama CHADEMA tunao ushahidi na tulitegemea Serikali ijibu hoja na si kuleta vihoja na kama hakuna ukweli Serikali ilipaswa kukanusha kwa ushahidi na vielelezo.

- Hatuwezi pata Bilioni 87 kwa kumuweka Lissu ndani.

- Serikali ilipaswa kujitokeza hadharani na kujibu shutuma hizi kwa hoja za msingi.

- Hadi leo hii, siku nne baada ya tamko hakuna hoja za kupinga toka Serikalini.

- Kwanini baada ya hukumu tulichelewa kulipa ilhali tulishindwa na hatukukata rufaa?

- Pia ijulikane ni nani alisababisha hili ili achukuliwe hatua na Awamu hii inayojua kuwajibisha wazembe.

- Hoja hii lazima ijibiwe ili kumsafisha Rais wetu.

- Mpaka sasa Lissu sijui Serikali itamfanya nini. Kauli ya Serikali iliyotolewa kwamba Lissu ni adui na Mhujumu na sawa na Mhaini inamletea shida na ana tishio la maisha yake.

- Kuna wananchi kwenye mitandao ya kijamii wanaamini Lissu ana hatia na wapo waliofikia kusema wanataka kumuua.

- Hii ni mara ya 11 Lissu anakamatwa. CHADEMA tuna kesi zaidi ya 300 za Wanachama, Viongozi na Wafuasi wetu na hazina kichwa wala miguu na IGP anaangalia na Waziri wa Mambo ya Ndani amelala kabisaaa tofauti na zamani alipokuwa Wizara nyingine.

- Tumemwandikia barua IGP na DCI, kwa mujibu wa Sheria unatakiwa kupewa dhamana isiyo na masharti magumu. Polisi wanaamua tu dhamana iwe milioni 12,20,1....ni kwa sheria ipi?

- Polisi wanapenda kusema ni agizo kutoka juu. Je agizo kutoka juu ni wapi huko? Tunataka tujue ili neno hilo lisitumike vibaya na watendaji wa Polisi kutaka kugandamiza watu.

- Haya mambo yanamtia aibu Rais kama maagizo haya hayatoki kwake. Anapaswa kuchukua hatua kuhusu hilo.

- Na kama ni maagizo kutoka kwa Rais kunatakiwa kuwe na ushahidi wa maandishi.

Katika barua hii tumetaka mambo yafuatayo:-

1. Ufafanuzi wa "Agizo kutoka juu". Inatoka kwa nani?

2. Ufafanuzi kuhusu double standards(Wabunge wa Upinzani kuwa matatani na wa CCM kuachwa huru kwa kufanya vitendo vilevile) na kama Jeshi linafanya kazi ya siasa tujue.

3. Tuelezwe kama kuwa mpinzani Tanzania ni kosa la jinai na kama kukosoa/kushauri/kuonya Serikali ni kosa la jinai.

4. Kwanini viongozi wa Upinzani hasa CHADEMA ndio wanakamatwa sana. Je ni wasumbufu sana? Wahalifu au?

5. Ni yupi mwema na yupi mwenye hatia kati ya waliotia hasara ya Bil 307 za Escrow, Bil 38 za mkataba kati ya Polisi na Lugumi na aliyesema tu kuwa "pesa zetu zinapotea"?

Tunasema kuwa Lissu aachiwe na badala yake akamatwe Ngeleja ambaye kwa mujibu wa Sheria kifungu cha 311 cha Sheria ya Makosa ya Jinai amekutwa na mali ya wizi. Amekutwa na fedha zilizopatikana kwa wizi, udanganyifu na kinyume na sheria. Ushahidi uko wazi na alikiri.

Pia wakamatwe Chenge, Tibaijuka, Werema na Paying Master General wa Wizara husika ktk mchakato wa pesa. Nchi hii inataka kuonesha mwizi wa kuku adhabu yake ni kifo, kifungo lakini wanaoiba kwa kuvaa suti hawapewi adhabu.

- Ikiwa hatutojibiwa barua yetu wala hatua hazitochukuliwa tutafanya yafuatayo:-

1. Tutaratibu maandamano ya Amani nchi nzima 31.08.2017. Itaitwa Black Thursday. Lengo litakuwa kushinikiza haki za kisiasa, kiuchumi, Utawala wa Sheria na Haki za Binadamu zitekelezwe kwa usawa.

2. Tutaratibu na kuwafundisha vijana wetu nchi nzima namna ya kulaani matendo ya uvunjifu wa sheria, uonevu na upendeleo popote yanapofanyika nchini kwa mujibu wa sheria ikiwa ni pamoja na kulinda chama, viongozi wetu na rasilimali zetu. Tutalichukua jukumu hili maana Jeshi litakuwa limeshindwa.

3. Tutasaidia Polisi kuwakamata watuhumiwa wa Escrow(maana wako nchini) kwa mujibu wa kifungu cha 16 cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai ya 2002 "Arrest by private person". Hata raia wa kawaida anaweza kumkamata mtu. Tutawafikisha polisi ili warudishe fedha tuweze kulipa deni letu na Bombardier ije nchini itusaidie wananchi wote.

No comments:

Post a Comment

Popular