Mtu mmoja auawa kwa kupimwa na bomuna wengine 13 kujeruhiwa wakiwemo askari wawili mkoani Manyara - KULUNZI FIKRA

Sunday, 30 July 2017

Mtu mmoja auawa kwa kupimwa na bomuna wengine 13 kujeruhiwa wakiwemo askari wawili mkoani Manyara

Mtu mmoja aliyejulikana kwa jina la Nembles Mbatia ameuawa kwa kupigwa bomu na wengine 13 kujeruhiwa vibaya wakiwemo askari wawili wa jeshi la polisi wakati wa vurugu za kugombea mpaka wa eneo la kuchimba madini ya Tanzanite kati ya kampuni ya Germ and Rock na Tanzanite One baada ya pande hizi kukutana chini ya ardhi kitengo kinachojulikana kama MTOBOZANO.

Eneo la Marelani lililoko wilayani Simanjiro mkoani Manyara ndio eneo pekee ambalo madini hayo hupatikana.

Tatizo la wachimbaji wadogo na wakubwa kukutana chini ya ardhi wakati wa kuchimba madini hayo limekuwa sugu sasa. Kutokana na sheria ya uchimbaji wa madini hayo ambayo huelekeza kuchimba kwa wima, jambo ambalo likipingwa na wachimbaji wadogo kutokana na mkao wa mikanda ya madini hayo ardhini.

Kufuatia vurugu hizi za takriban siku tatu mfululizo, Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Manyara Alfred Masawe analazimika kuweka kambi katika eneo la mgogoro kuhakikisha amani ina tamalaki tena katika eneo hilo huku alithibitisha kifo cha Nembles na majeruhi.

Kufuatia hali hii, kwa haraka Kamishna msaidizi wa madini kanda ya Kaskazini Adam Komba atazikutanisha pande zote za mgogoro huu huku akishirikisha kamati ya ulinzi na usalama wilaya ya Simanjiro.[​IMG]

Na hapa wanatoa msimamo wa kilicho afikiwa kwa pamoja ikiwemo hatua ya kusitisha shughuli za uchimbaji kwa muda eneo la mgogoro.

Chanzo: ChannelTen

No comments:

Post a Comment

Popular