Lema asema wakati wa kikwete ccm ilijibu wapinzani jukwaani. - KULUNZI FIKRA

Saturday, 29 July 2017

Lema asema wakati wa kikwete ccm ilijibu wapinzani jukwaani.

Mbunge wa arusha mjini(chadema) Mhe Godbless Lema ameendelea kukumbuka utawala wa serikali ya awamu ya NNE,akisema ulikuwa ukijibu hoja za wapinzani jukwaani,badala ya kutumia dola kama ulivyo utawala wa sasa.
Lema,ambaye ameingia katika misukosuko na vyombo vya dola kutokana na kauli zake,pia amesema hatanyamaza licha ya kushauriwa afanye hivyo na baadhi ya watu baada ya kukaa mahabusu kwa takribani miezi mienne mapema mwaka huu kutokana na pingimizi la dhamana yake kuchelewa kuamuliwa.
Lema,alisema wakati wa awamu hiyo katibu mkuu wa ccm,Abdalarhman Kinana na Aliyekuwa katibu wa itikadi na uenezi,Nape Nnauye walikuwa wakijibu hoja za upinzani jukwaani.
Amesema hayo juzi alipokuwa akizungumzia demokrasia wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika kata ya Osunyai jijini Arusha.

No comments:

Post a Comment

Popular