Kamati kuu ya chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) imekutana kwa siku mbili 29-30 July, katika hotel ya Double Tree, Jijini Dar es Salaam
kikao hicho kimejadili na kufikia maamuzi na hatua za kuchukua katika ajenda zifwatazo
1: Hali ya mwenendo wa siasa katika nchi na ukandamizaji wa demokrasia unaofanywa na serikali ya awamu yatano
2: Kuporomoka kwa uchumi na hali ngumu ya maisha kwa Watanzania
3: kamata kamata inayoendelea kufanywa na vyombo vya dola dhidi ya viongozi, wanachama na wafuasi wa Chadema maeneo mbalimbali nchi nzima.
Taarifa kamili juu ya maazimio hayo na hatua zitakazochukuliwa na chama itatolewa kesho Jumatatu tarehe 31 July 2017, kwenye kikao na waandishi wa habari kitakachofanyika jijini Dar es Salaam
Imetolewa na
John Mrema
Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje
No comments:
Post a Comment