Wabunge Susan Kiwanga na Peter Lijualikali waliofikishwa Mahakama ya Hakimu mkazi mkoani Morogoro pamoja na wafuasi wengine 36 wamerudishwa rumande.
Mahakama ilikuwa itoe uamuzi wa dhamana leo Jumanne Desemba 5, 2017 imekwama kufanya hivyo kutokana na kuibukahoja za kisheria.
Upande wa mashtaka na ule wa utetezi umevutana kuhusu hati ya kiapo cha kupinga dhamana iliyowasilishwa mahakamani hapo leo.
Kutokana na mvutano wa kisheria, Hakimu Ivan Msack ameamua kuahirisha kesi hiyo hadi kesho Jumatano Desemba 6, 2017 ili kuweza kutoa fursa kwa pande zote mbili kujibu hoja kuhusu hati hiyo.
Washtakiwa wote wanakabiliwa na mashtaka nane likiwamo la kuchomwa moto ofisi ya kata ya Sofi iliyopo Wilayani Malinyi.
Washtakiwa hao wote wanatetewa na mawakili Peter Kibatala, Ignaz Punge, Frederick Kiwelo na Bartholomew Tarimo.
Upande wa mashtaka unawakilishwa na mawakili wa serikali Edga Bantalaki na Sunday Hyera.
Pia mwenyekiti wa chadema, Freeman Mbowe na mjumbe wa kamati kuu ya chama hicho Mhe Frederick Sumaye walihudhuria mahakamani hapo.
Pia wabunge hao walifanikiwa kuhudhuria mahakamani hapo ni Mbunge wa Tarime vijijini, Mhe John Heche pamoja na Mbunge wa viti maalum, Mhe Devota Minja.

No comments:
Post a Comment