Vigogo wa chama cha mapinduzi (CCM) wapigana vikumbo jimboni kwa Nyalandu. - KULUNZI FIKRA

Friday, 8 December 2017

Vigogo wa chama cha mapinduzi (CCM) wapigana vikumbo jimboni kwa Nyalandu.

Vikumbo vya kuwania ubunge katika majimbo ya Singida Kaskazini, Longido na Songea mjini vimeanza kwa idadi kubwa ya makada wa chama cha mapinduzi (CCM) kujitokeza kuchukua fomu.

Katika jimbo la Singida Kaskazini ambalo liko wazi baada ya Lazaro Nyalandu kujiuzulu na kujivua uanachama wa chama cha mapinduzi (CCM) kisha kuomba kujiunga na chadema oktoba 30 kwa madai ya kutoridhishwa na mwenendo wa ndani wa chama hicho tawala. Tayari wagombea 17 wamejitokeza kuchukua fomu akiwamo Aliyekuwa msaidizi wake.

Kwa mujibu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) majimbo hayo yatafanya Uchaguzi January 13 mwakani na mchakato wa kupata wagombea ndani ya CCM ulianza toka Desemba 5 na unatarajia kukamilika kesho.

Katibu wa chama cha mapinduzi (CCM) wilaya ya Singida vijijini, Grace Shindika alisema jana kuwa miongoni mwa wanachama waliojitokeza kuchukua fomu kwaajili ya kuwania nafasi ya ubunge ni  Elia Digha ambaye ni mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya.

"Watu wamejitokeza kwa wingi kuwania nafasi hii kuliko ilivyokuwa katika Uchaguzi mkuu wa mwaka 2015. Karibu wote wamechukua na kujaza fomu kisha kurejesha isipokuwa wanachama wawili tu ndiyo hawajaresha fomu zao", alisema Grace.

Grace alisema hakuwa tayari katika nafasi ya kutaja majina ya  wanachama wote walichukua fomu kwaajili ya kukiwakilisha chama katika uchunguzi huo na kwamba miongoni mwao pia ni Aliyekuwa mwenyekiti wa CCM wilaya ya Singida vijijini, ndugu Narumba Hanje.

Mwanachama mwingine aliyejitokeza kutaja kupewa ridhaa ya CCM kuwania jimbo hilo ni Haidal Gulamali ambaye al8wahi kuwa katibu wa uchumi na fedha wa CCM mkoani Dodoma, pia Gulamali aliwahi kuwania kuteuliwa na chama cha mapinduzi (CCM) kugombea ubunge jimbo la Dodoma mjini mara mbili bila mafanikio.

Kwa mara ya kwanza Gulamali aliingia katika mchakato wa ndani ya chama cha mapinduzi (CCM) kuwania ubunge was jimbo la Dodoma mjini kwenye uchunguzi wa mwaka 20101 ambapo alishika nafasi ya saba kati ya wagombea kumi na moja na katika Uchaguzi wa mwaka 2015 alishika nafasi ya pili.

Kwa majimbo ya Songea mjini na Longido.

Katika jimbo la Songea mjini tayari wanachama wa chama cha mapinduzi (CCM) wameshachukua fomu za kugombea ubunge kuziba nafasi iliyotokana na kifo cha Leonidas Gama aliyefariki dunia Novemba 23.

Akizungumza na kulunzifikra blog jana katibu wa CCM wilaya ya kichama ya Songea mjini, Juma Mpele alisema wanachama hao wote wamechukua fomu tangu juzi na jana mchana ,huku akibashiri kwamba wanachama wengi zaidi wanatarajia kujitokeza kuwania nafasi hiyo.

Pamoja na kutangazwa tarehe ya Uchaguzi katika jimbo la Longido kujaza nafasi Aliyekuwa Mbunge wake kupitia chadema Onesmo Ole Nangale hadi jana hakuna wana-ccm aliyejitokeza kuchukua fomu za kuwania ubunge katika jimbo hilo. Ole Nangale alivuliwa ubunge baada ya mahakama kuu kutengua ushindi wake kutokana na kasoro kadhaa zilizojitokeza katika Uchaguzi wa mwaka 2015.

No comments:

Post a Comment

Popular