Polepole amjibu Lowasa kuhusu kumsamehewa kwa babu Seya. - KULUNZI FIKRA

Sunday, 10 December 2017

Polepole amjibu Lowasa kuhusu kumsamehewa kwa babu Seya.

 Hizi habari zipuuzwe zipuuzwe katika kiwango kikuu kabisa kwa sababu kwanza mtu ambaye amesema hana uhalali kwa alichokisema. Ni mtu ambaye hivi karibuni wamekuwa na mtu wa kudandia hoja kila jambo zuri linalofanywa amekuwa akidai kuwa yeye ndio muasisi wa jambo hilo, mtu anayeshindwa mara zote hupenda kuchuka sifa hata katika mambo yasiyomuhusu." Anasema Polepole

"Nikizungumzia hili la ndugu rais kusamehe wafungwa, mchakato wa kusamehe wafungwa upo kwa mujibu wa katiba na wafungwa wamekuwa wakisamehewa baada ya kukidhi vigezo fulani muhimu. Kwamba mchakato wake umekidhi masharti ya msingi ambayo mtu naweza kusamehewa. Rais amepewa mamalaka hayo kikatiba kwa mba anamsamehe mtu ambaye ameona anastahili msamaha baada ya mchakato maalumu madhubuti kabisa kukamilika" anaendelea kusema Polepole


"Hili sio jambo la kubahatisha jambo la mtu kusema amemshawishi rais. Huyu mzee ambaye amezungumza kuwa hii ilikuwa ni ahadi yake wakati wa kampeni ni mzee ambaye amehudumu kwenye serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kipindi Babu Seya anafungwa huyu mzee alikuwa Waziri Mkuu, tena hakuwa waziri Mkuu bali waziri mkuu mwenye nguvu sana, kama alijua Babu Seya labda hakutendewa haki kwa namna yoyote kwa fikra zake angaliweza kumshauri rais wake kwa kipindi hicho kuwa huyu mtu hastahili kufungwa asamehewe" amesema Polepole.

"Kashindwa kuzuia asifungwe, kashindwa kwa miaka mingi kumshawishi rais wake amsamehe. leo mtu ambaye hakuwa sehemu ya uamuzi wala hakuwa na sehemu nyeti katika serikali, Ndugu Magufuli kipindi hicho alikuwa waziri wa kawaida tu, baada ya tafakuri ya kina na tathini yadidifu ya miaka miwili akaon akatika watu wamejirudi na kustahili msamaha. Huyo mzee anaibuka, aache tabia za kizandiki na kinafki watanzania wanataka upinzani unaojenga hoja na sio unaorukia hoja zisizowahusu"

No comments:

Post a Comment

Popular