Masheikh watano akiwemo Mwenyekiti wa Halmashauri ya Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA), mkoani Katavi, Sheikh Shaban Bakari wamejiuzulu uongozi wakidai kuwepo kwa migogoro ya uongozi na ukiukwaji wa Katiba ya Bakwata.
Halmashauri ya baraza hilo inaundwa na viongozi sita ambao ni Masheikh, watano kati yao ndio waliotangaza kujiuzulu ambao ni Mwenyekiti wao Sheikh Bakari, Sheikh Mashaka Kakulukulu, Sheikh Hassan Mbaruku, Sheikh Said Haruna Omary na Sheikh Mohamed Sigulu.
Wakitangaza uamuzi huo jana mjini Katavi mbele ya waandishi wa habari, Sheikh Kakulukulu alisema haoni sababu ya kuendelea kuwa kiongozi wa halmashauri ya baraza hilo akidai kumekuwepo na baadhi ya mambo ya hayaendi sawa.
"Hata Katiba ya Bakwata imekuwa ikikiukwa na kusababisha migongano ya kimaslahi, hata utekelezaji wa miradi ya maendeleo umekwama kutokana na msuguano wa kiuongozi", alisema Sheikh Kakulukulu.
Kauli hiyo iliungwa mkono na Masheikh wengine, huku Sheikh Sigulu akidai kuwa msuguano uliopo wa kiuongozi ndani ya Bakwata umesababishwa na mwalimu wa madrasa katika Msikiti Mkuu mjini Mpanda kuamua kuacha kazi ya kufundisha hivi karibuni.

No comments:
Post a Comment