Katibu wa kamati ya maadili ACT-wazalendo mkoa wa Kigoma amejiuzulu. - KULUNZI FIKRA

Thursday, 7 December 2017

Katibu wa kamati ya maadili ACT-wazalendo mkoa wa Kigoma amejiuzulu.

 
                                        TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

                                               07-12-2017
                                                 KIGOMA

Mimi Wilson Elias Mwambe, Katibu wa kamati ya maadili mkoa wa Kigoma, na Katibu wa mipango na chaguzi kata ya Mwanga kusini, jimbo la Kigoma mjini kwa hiari yangu nimeamua kujiudhulu nafasi zangu zote za uongozi nilizokua nashikilia ndani ya chama cha ACT Wazalendo.

Nimefanya uamuzi huu Leo tarehe 07-12-2017 kwa utashi wangu na bila shinikizo la mtu yeyote.

Sababu za kufanya hivi ni kutokana na Manispaa ya Kigoma ujiji ilio chini ya chama cha ACT Wazalendo kushindwa kuwalipa wenyeviti wa mitaa posho zao kwa miaka miwili sasa; Uongozi wa mkoa wa Kigoma, uongozi wa jimbo la Kigoma mjini kukiuka malengo thabiti ya chama ambao ni kupigania maslahi ya Taifa kwanza; Kuminya uwazi " Transparency " kuwanyima madiwani, na wanachama Uhuru na haki yao yakutoa maoni na asa kwenye sakata nzima ya kiwanja " Kitalu 2 PB" chenye mgogoro kati ya Manispaa ya Kigoma ujiji na mwekezaji SHEIN/ kata ya Rusimbi; Kukanyaga kwa makusudi ahadi nambari moja ya mwanachama wa ACT Wazalendo " 1. Nitapambana dhidi ya dhuluma, fitina, unafiki, Uongo, Rushwa na ufisadi kwa uwezo wangu wote"

Kwakua nia yangu ilikua ni kuipigania maslahi mapana ya Taifa kwanza, na muelekeo wa chama kwasasa unaonekana kua tofauti, sioni sababu za kuendelea kua kiongozi ndani ya chama kinachopinga falsafa, itikadi, na misingi iliokiasisi.

Na kwakua niliwahi andika barua kwa Katibu wa jimbo la Kigoma mjini mnamo tarehe 13-02-2017 iliokua na nakala kwa :
- Katibu wa Mkoa
- Meya wa Manispaa ya Kigoma ujiji,
- Mbunge wa jimbo la Kigoma mjini

Kuomba usuluhisho kwenye internal conflict/ mradi wa Katosho, na hadi Leo sikuwahi jibiwa wala kuitwa ili kusikilizwa ( Weakest administration), sikuona sababu za kutuma barua yangu tena uko.

Niwashukuru viongozi na wanachama wa ACT Wazalendo wote kwa ushirikiano mzuli mulonipa toka 2014 hadi 2017 bila kujali mapungufu, na madhaifu yangu.

Nimshukuru vile vile mhe. Zitto Zuberi KABWE, Mbunge kwa kuona capacity, ability, importance yangu na kuamua kuniweka campaign manager wake kwenye mapambano yakulisaka jimbo la Kigoma mjini mwaka 2015.

Nimalizie tu kwakutoa ushauri kwa Mbunge, Meya, madiwani, viongozi mbali mbali wa chama na wanachama wote wa ACT Wazalendo kuheshim, kudumisha na kuipigania falsafa, itikadi, na misingi iliokiasisi chama, maana inatoa privilege kubwa kwenye maslahi mapana ya Taifa kwanza.

Mungu ibariki Tanzania, Mungu tubariki Watanzania.

-------------------------

Wilson Elias Mwambe
+255 754-553451

No comments:

Post a Comment

Popular