Mahakama ya Hakimu makazi mjini Dodoma ilitoa uamuzi wa maombi ya dhamana ya Aliyekuwa mwenyekiti wa umoja wa vijana CCM (UVCCM), ndugu Sadifa Juma Khamisi anayekabiliwa na makosa mawili ya Rushwa.
Uamuzi huo unatokana na upande wa mashtaka kuwasilisha hati ya kiapo kuzuia dhamana kwa madai ya kuvurugwa upelelezi na kuingilia uchaguzi wa UVCCM ambao uliofanyika jana jumapili Desemba 10, 2017 katika ukumbi wa chuo cha mipango mjini Dodoma.
Akisoma hati ya mashtaka mahakamani hapo wakili wa Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (Takukuru), Biswalo Biswalo amedai kuwa ndugu Sadifa anashtakiwa kwa makosa mawili.
Katika shtaka la kwanza amedai Desemba 9, 2017 katika makazi yake kwenye kata ya mnada mjini Dodoma akiwa mwenyekiti wa UVCCM Taifa na muajiri wa umoja huo, aliwahonga wajumbe ili waweze kumchagua Rashid Mohamed Aliyekuwa akiwania nafasi ya makamu mwenyekiti katika uchaguzi mkuu wa umoja huo.
Ndugu Sadifa katika shtaka la pili amedaiwa katika eneo hilo hilo na siku hiyo hiyo aliwahidi wajumbe kuwalipia usafiri wa kuwasafirisha kutoka Dodoma mpaka Kagera kama zawadi ili waweze kumchagua Rashid Mohamed Aliyekuwa akiwania nafasi ya makamu mwenyekiti wa UVCCM Taifa katika uchaguzi huo.
Wakili Biswalo amesema hati ya kiapo iliyotolewa na kamanda wa Takukuru mkoa wa Dodoma, Emma Kuhanga kupinga maombi ya dhamana kwa sababu endapo atapewa dhamana atavuruga upelelezi na kuingilia uchaguzi wa UVCCM Taifa.
Wakili wa upande wa utetezi, Godfrey Wasanga amepinga hoja hiyo alisema makosa aliyoshtakiwa nayo mteja wake hana dhamana na hawezi kuingilia uchaguzi wa UVCCM Taifa kwa kuwa umeshafanyika na washindi wameshatangazwa.
Kutokana na mabishano hayo, Hakimu mfawidhi wa mahakama ya Hakimu mkazi Dodoma, Emmanuel Favo aliamua kuahirisha kesi hiyo hadi Desemba 19, 2017 kutoa nafasi kwa mahakama kupitia kiapo kilicholetwa na upande wa mashtaka ili kutoa haki katika maombi ya dhamana ya mshtakiwa.
Kutokana na hali hiyo ndugu Sadifa amerejeshwa rumande.

No comments:
Post a Comment