Chama cha demokrasia na maendeleo Chadema kipo hatarini kupoteza Halmashauri ya Wilaya ya Monduli, baada ya kupoteza madiwani saba kati ya 17 waliokuwa wakiongoza kata mbalimbali.
Madiwani hao walijiuzulu nafasi zao na kujiunga na CCM ambayo kwa sasa ina madiwani kumi, hivyo kufanya vyama hivyo kuwa na idadi sawa ya madiwani.
Madiwani wa Chadema, wamejiuzulu ndani ya siku tatu.
Baadhi ya madiwani wa Chadema ni wale waliohama kutoka CCM wakidai wanamuunga mkono aliyekuwa mgombea wa urais kwa tiketi ya Chadema, Edward Lowassa.
Awali, Lowassa alikuwa mbunge wa Monduli (CCM).
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Monduli, Stevin Ulaya alisema jana kuwa amepokea barua za madiwani saba kujiuzulu akiwamo aliyekuwa makamu mwenyekiti wa halmashaur hiyo, Edward Lenenu ambaye alikuwa diwani wa Naalarami.
“Nimepokea barua za madiwani saba kujiuzulu na wana sababu tofauti, lakini kubwa ni kuunga mkono Serikali,” alisema Ulaya.
Madiwani wengine waliojiuzulu ni Solomon Mollel wa Lolkisale na Loith Mollel wa Meserani ambao walipokewa jana na mwenyekiti wa CCM Mkoa Arusha, Loota Sanare.
Wengine ni diwani wa Monduli Juu, Bariki Sumuni; Diwani wa Migungani, Benedict Mawalla; Diwani wa viti Maalumu, Enoti Leringa; na diwani wa Engutoto, Abroce Mtui.
Mbunge wa jimbo la Monduli, Julias Kalanga alisema tayari amepata taarifa ya kujiuzulu kwa madiwani hao saba. “Ni kweli ndani ya siku tatu madiwani saba wamejiuzulu sababu zao nyingi si za msingi ila tunafuatilia kujua kinachoendelea,” alisema.
Hata hivyo, Kalanga alisema kuwauamuzi wa kujiuzulu kwa madiwani hao hakuwezi kuhitimisha uongozi wa Chadema katika halmashauri kwa kuwa uchaguzi wa mwenyekiti hauwezi kufanyika bila kuwapo sababu za msingi.
“Lakini kwa sasa sina maoni zaidi, ngoja tusubiri kitakachotokea ila bado udhibiti wa halmashauri ni wa upinzani,” alisema Kalanga.
Lowassa ahamia Chadema
Julai 28, 2015, Lowassa ambaye ni Waziri Mkuu wa zamani alitangaza rasmi kuihama CCM na kujiunga na Chadema baada ya kukatwa kwenye mchakato wa kuwania urais ndani ya chama hicho kikongwe.

No comments:
Post a Comment