Waziri wa Tamisemi Seleman Jafo ametoa maagizo kwa wakuu wa Mikoa. - KULUNZI FIKRA

Wednesday, 21 March 2018

Waziri wa Tamisemi Seleman Jafo ametoa maagizo kwa wakuu wa Mikoa.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa,  Mhe Selemani Jafo amewataka wakuu wa mikoa nchi nzima kusimamia utekelezaji wa bajeti ya mwaka 2017/18 katika kipindi kilichobaki ili kutekeleza miradi ya maendeleo iliyopangwa kufanyika.

Mhe Jafo ametoa agizo hilo wakati wa kikao kazi cha kujadili sura ya bajeti ya mwaka 2018/19 kilichokutanisha wakuu wa mikoa 26 na makatibu tawala wa mikoa.

Pia Mhe Jafo alisema ikiwa imebakia miezi michache kukamilisha bajeti hiyo, kuna fedha za maendeleo zinazoendelea kutolewa ni vyema zikasimamiwa ipasavyo ili kukamilisha na kutekeleza miradi hiyo.

"Tunaelekea mwisho wa utekelezaji wa bajeti na kuna fedha za maendeleo zinatumwa, niwaombe wakuu wa mikoa mkasimamie vyema fedha na utekelezaji, ili ikifika Juni 30, mwaka huu kile kilichopangwa kutekelewa kiwe kimetekelizwa,” alisema Mhe Jafo.

Aidha, Mhe Jafo pia aliwataka wakuu wa mikoa kwenda kuweka sawa na kuzijua bajeti zao ili kutoleta shida pindi mikoa itakapokutana na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti.

"Katika miaka miwili ya utekelezaji wa bajeti, nimebaini matatizo kadhaa, baadhi ya mikoa ilikuwa inafika kwenye kamati wakiwa hawajajiandaa na hata randama zilizoandaliwa zinakuwa tofauti na zile zilizopelekwa Hazina," alisema Mhe Jafo.

No comments:

Post a Comment

Popular