Walimu wa shule za msingi na sekondari wa Kata ya Kijichi Mkoa wa Dar es Salaam, wameahidiwa kufanyiwa ziara ya mapumziko mafupi baada ya muda wao wa kazi ili kujenga na kuimarisha afya zao kwa kupumzisha akili na kubadilishana mawazo kutoka kwa walimu wa shule zingine.
Mbali na hilo, pia Walimu hao wamewekewa mkakati maalum wa kuinua ufaulu kwa wanafunzi wao ambapo walimu watakaofanikiwa kufaulisha wanafunzi wengi watatunukiwa tuzo zitakazopewa jina la Diwani Award.
Hayo yamesemwa na Diwani wa Kata ya Kijichi kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Elias Mtarawanje, wakati akizungumza na walimu wa kata hiyo kwenye Shule ya Msingi Mtoni Kijichi Wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam.
Diwani huyo amesema pia yupo mbioni kuanzisha mashindano ya wanafunzi ya kimasomo na kwa watakaofanya vizuri watapatiwa zawadi, lengo likiwa ni kuongeza ari ya kuongeza ufaulu wa kimasomo.
Mtarawanje, amesema atahakikisha walimu waliopo katika kata yake wanafanya safari kwa kutoka nje ili kubadili mazingira kila mwisho wa mwaka na lengo likiwa ni kubadilisha fikra na akili baada ya kukabiliwa majukumu ya kikazi na kupata nguvu za kufundisha wanaporudi shuleni na kuleta matokeo chanya kwa maendeleo ya taifa.

No comments:
Post a Comment