Rais Dkt John Pombe Magufuli amewataka maaskofu kuhubiri kuhusu ujenzi wa viwanda nchini ili Tanzania isinunue dawa nje ya nchi.
Rais Magufuli alitoa kauli hiyo Dar es Salaam Jana wakati wa hafla fupi ya kukabidhi magari 181 kwa Bohari Kuu ya Dawa (MSD), ya kusambaza dawa maeneo mbalimbali nchini.
“Lakini hili tumezungumza, tunaimba, sijui nitumie lugha gani, labda niwaombe maaskofu wajaribu kuhubiri hili kwamba tunahitaji kutengeneza viwanda ili Watanzania wapate ajira", alisema Rais Magufuli.
“Labda niwaombe wahubiri na Watanzania wengine wanaojua kuhubiri vizuri, tuwaeleze Watanzania kwamba tunapoteza Sh bilioni 500 kila mwaka kununulia dawa na vifaa mbalimbali kutoka nje wakati tenda hizi zingebaki hapa", alisema Rais Magufuli.
“Kwa bahati nzuri Global Fund wametupa tenda ya nje ya Tanzania kununua dawa pia ya nchi zote za SADC, lakini tunalalamikia mengine, yale ya maana kwa manufaa ya Watanzania hatuyalalamikii", alisema Rais Magufuli.
“Sijui Watanzania tumelogwa! Basi huyo shetani tumkemee kwa majina yote, jina la Muhammad na Yesu, huyo shetani akashindwe ili Watanzania tujue mahali gani tunatakiwa kwenda,” alisema Rais Magufuli.
Katika hafla hiyo, Rais Magufuli alisema sekta ya afya ni nyeti na muhimu na kwamba bila sekta hiyo ni ndoto kufikia maendeleo ya nchi.
“Vifaa plastic (gloves) tunaagiza nje, mabomba ya sindano tunaagiza nje, tungekuwa na viwanda vyetu hizi Sh bilioni 500 zingerudi hapa, tungekuwa na viwanda hizi fedha Sh bilioni 269 zinazopitishwa na Bunge kwa ajili ya kununulia dawa zingebaki hapa na kutengeneza ajira", alisema Rais Magufuli.
“Inauma ukusanye pesa kwa watu masikini, mama lishe, wafanyabiashara ndogondogo halafu hizo pesa mnapeleka kwa wawekezaji nje kununua dawa, mnaenda kutengeneza ajira kwa ajili ya wengine, mimi si mbaguzi, lakini hili linaniuma. Sisi tunakuwa ni chombo la kukusanya fedha kwa ajili ya wengine", alisema Rais Magufuli.
“Nawapongeza wafanyakazi wa MSD kwa sababu wakati naingia madarakani mahali palipokuwa na changamoto kubwa ni MSD, waziri kila siku alikuwa ananiambia. Mmeanza vizuri, mimi ni mgumu kupongeza, kweli mmefanya kazi nzuri sana", alisema Rais Magufuli.
“Niliwaambia mfungue maduka lakini msiwape halmashauri, kama ni wafanyakazi waongezeni lakini si kuwapa tena halmashauri, zitapotea. Mimi ninawafahamu TAMISEMI na ndiyo maana nikasema hata dawa ziende moja kwa moja katika hospitali", alisema Rais Magufuli.
“Mkurugenzi nakupongeza sana, najua ulipigwa madongo nikanyamaza, waache wakupige madongo, wewe ndio mkurugenzi wa MSD,” alisema Rais Magufuli.
Pia Rais Magufuli alisema kupatikana kwa magari hayo kumeifanya MSD kuwa na magari 213 kutoka 32 waliyokuwa nayo awali.

No comments:
Post a Comment