Profesa Lipumba afunguka mengi juu ya Maalim Seif. - KULUNZI FIKRA

Sunday, 18 March 2018

Profesa Lipumba afunguka mengi juu ya Maalim Seif.

 
Mwenyekiti wa CUF anayetambuliwa na Msajili wa Vyama vya Siasa, Profesa  Ibrahim Lipumba amesema CUF  sana Katibu mkuu wake, Maalim Seif Sharif Hamad kwa kudhani kuwa kama angepata yeye basi wamepata wote  kumbe ni tofauti kitu ambacho waliwakosea Wazanzibar.

Profesa Lipumba ametoa kauli hiyo leo wakati akifungua kikao cha kwanza cha kawaida cha Baraza Kuu la Uongozi la CUF kilichofanyika katika makao makuu ya chama hicho, maeneo ya Buguruni jijini Dar es Salaam.

Ameongeza kuwa hali ya kumdekeza Maalim  Seif imesababisha CUF kushindwa kupata viongozi watakaoingia katika Baraza la Wawakilishi la Zanzibar na kutokuwepo kwenye Serikali ya Umoja wa Kitaifa.

“CUF tumemdekeza kwa muda mrefu na zile nyimbo tulizokuwa tukiimba ya kuwa akipata Seif tumepata sote zilikuwa zimemuingia kichwani kwelikweli na yeye alitafsiri kuwa akikosa Seif tumekosa sote",amesema Profesa Lipumba.

"Matokea yake tumekosa kuwa na uwakilishi katika Baraza la Uwakilishi jambo ambalo limetuathiri kisiasa hasa Zanzibar. Hili kosa kubwa tuliowakosea Wazanzibari” amesema Profesa Lipumba.

No comments:

Post a Comment

Popular