Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu amemtaka meneja Tanesco Mkoa wa Pwani, Martin Madulu kufanya uchunguzi kumbaini mtumishi wa shirika hilo, aliyemtaka mkazi wa Kibaha ashiriki katika maandamano ya Mange Kimambi, Aprili 26 ndipo apate umeme.
Alitoa agizo hilo Machi 26 katika Mtaa wa Sagale, Magengeni, Kata ya Viziwaziwa, Kibaha baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa mkazi wa eneo hilo, Bebronia Meteli, “Naomba meneja Tanesco unipe taarifa ya madai haya na majina ya wasoma mita eneo hilo na uchunguzi utaanzia hapo mara moja na tukijiridhisha ni kweli yupo mtumishi huyo, basi tutamshughulikia ipasavyo.”
Meteli alitoa malalamiko hayo katika mkutano wa hadhara akilalamika kuwa wakazi wa eneo hilo hawajapata umeme wa Wakala wa Nishati Vijijini (Rea) awamu ya pili licha ya kuwa wapo kwenye orodha hiyo. Alisema hawajawekewa nguzo, hivyo kulazimika kuomba kuwekewa umeme wa kawaida wa Tanesco na ndipo alipokutana na majibu ya kukatisha tamaa.
“Waziri tunashukuru umekuja leo, kutokana na kutambua umuhimu wa nishati, mimi nilienda Tanesco kuomba angalau basi watuwekee umeme wa kawaida na nikajibiwa kama nahitaji umeme nikaandamane maandamano ya Mange,” alisema Meteli.
Mgalu alijibu, “Sitaki kuamini kama mtumishi wa Serikali anaweza kumwambia mtu akaandamane maandamano ya Mange, huko ni kuwaingiza wananchi kwenye mtego ambao hauna maana yoyote kwani mpango huo hautafanikiwa kamwe, kama huyo ni mwanamke kweli aje hapa live tumuone mbona sisi tupo live.”
Alisema hakuna huduma yoyote ya umeme itakayotolewa kwa sababu tu eti watu wameandamana, bali zitawafikiwa wote kulingana na vipaumbele vya mahitaji yaliyopo na bila ubaguzi wa aina yoyote.
Akizungumzia suala hilo, Madulu alisema gwaride la utambuzi wa mtumishi anayedaiwa kufanya hivyo bado halijafanyika kwa kuwa mlalamikaji ameshindwa kutoa vielelezo vitakavyosaidia kutambua ni kada ipi ya ofisi hiyo iliyohusika na kauli hiyo.
Madulu alibainisha kuwa katika maeneo ya miradi ya umeme ukiwamo ule wa kawaida, Rea na mingine, kuna mafundi na kandarasi tu na kwamba wasoma mita wa sasa, hawaitumii ofisi ya Tanesco kwa sababu wateja wengi wanatumia mfumo wa huduma ya umeme wa Luku.
“Sisi tupo tayari kutekeleza agizo la naibu waziri, lakini mlalamikaji ameshindwa kubaibisha mtumishi huyo ni wa kada ipi zaidi ya kusema anasoma mita. Sasa sisi Tanesco siku hizi hatuna wasoma mita maana tunatumia Luku,” alisema.
Hata hivyo, Madulu aliahidi kufanya gwaride la utambuzi wakati wowote pindi mlalamikaji atakapotoa ushirikiano kwa kuwa ofisi yake hailei watumishi wasio waadilifu.
“Hata sisi tumeshtuka kusikia kuna watumishi wanatumia changamoto zilizopo kuhamasisha watu waandamane, sio kanuni zetu na wala hatupaswi kumuomba mtu kitu, ili tumpe huduma bali tunapaswa kutoa huduma kwa kila raia kwa wakati kwa mujibu wa sheria zetu.” alisema.

No comments:
Post a Comment