Lori la mafuta limetumbukia mtoni kisha kuwaka moto. - KULUNZI FIKRA

Friday, 23 March 2018

Lori la mafuta limetumbukia mtoni kisha kuwaka moto.

 
Kamanda wa polisi mkoani Singida Deborah Magiligimba amesema kwamba, ajali hiyo imetokea saa nne na nusu asubuhi milima ya Senkenke Wilaya ya Iramba barabara ya Singida - Nzega.

Gari iliyohusika kwenye ajali hiyo ni namba T167 DTC aina ya Flight liner ambayo ilikuwa na Trailer namba T 960 ALS. Hili gari ni mali ya kampuni ya  Petromac Africa ya Jijini Dar es salaam.

Gali hii iliacha njia na kupinduka  ndani ya mto ambapo ililipuka na kusababisha moto mkubwa uliopelekea vifo vya watu wawili ambao ni wanaume.

Uchunguzi wa  awali wa Jeshi la Polisi baada ya kufatilia kwenye mzani wa Singida, gari ilipimwa mzani wa Singida saa moja na dakika  27 asubuhi.

Dereva wa gari hiyo alikuwa anaitwa Erasto Abedi Rusazi na alikuwa na tingo (msaidizi) wake anayeitwa Ramadhani Hashim Ramadhini wote ni Wakazi wa Tabata Jijini Dar es Salaam.

Pia kamanda Deborah Magiligimba, ametoa wito kwa madereva watii sharia za barabarani ili kuepusha ajali.

No comments:

Post a Comment

Popular