Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya nchini (DCEA), Rogers Sianga ameeleza namna kigogo na mfanyabiashara wa kemikali bashirifu, alivyotaka kumhonga Sh milioni 800.
Awali, Kamishna huyo alibainisha kuwa udhibiti wa dawa za kulevya unaoendelea sasa nchini, umesababisha baadhi ya wafanyabiashara kuanza kuingiza kemikali bashirifu na kuzalisha dawa za kulevya, huku soko lao likilenga wanafunzi wa shule za msingi na sekondari hususani wale wanaotoka kwenye familia zenye uwezo.
Sianga alisema hayo mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ukimwi na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu, Jenista Mhagama.
Akitoa taarifa ya utendaji wa mamlaka hiyo na namna ya kupambana na dawa za kulevya nchini kwa kamati hiyo, Siyanga alisema mbali na yeye kutaka kuhongwa, pia Kamishna wa Sheria wa Mamlaka hiyo, Edwin Kakolaki naye alitaka kuhonga Sh milioni 400 ili avuruge kesi asiweze kushtakiwa.
"Pamoja na jitihada za kutaka kutuhonga lakini kigogo huyo na mwenzake walikamatwa. Alitaka kumpa hongo kamishna Kakolaki ya Sh milioni 400 ili avuruge kesi, kwangu mimi alisema akinifikia atatoa Sh milioni 800," alieleza Sianga.
Aidha alisema kwa sasa wanakusudia kuendesha kesi za dawa za kulevya kwa kutumia waendesha mashitaka wao.
Akizungumzia bangi, Siyanga alisema: "Hali yetu ni mbaya, niseme tu kwa watu wanaolima bangi na mirungi tunaanza kufanya tafiti wa maeneo yanayolima zao hilo ili waanzishe kilimo mbadala wa mazao ya biashara ili waachane na dawa za kulevya,".
Alisema wameteketeza bangi Mkoa wa Arusha, wanakwenda mkoa wa Tanga, Morogoro, Iringa na watafika mikoa yote wakipitishiwa maombi ya bajeti wanayoiomba.
Sianga aliwahakikishia wabunge kuwa wamedhibiti uingizwaji wa dawa za kulevya nchini na kwamba njia iliyokuwa ikitumika kama Bahari ya Hindi wamedhibiti.

No comments:
Post a Comment