Serikali imesema ina mpango wa kushirikiana na waendesha pikipiki maarufu kama ‘bodabada’ ili kusafirisha sampuli ya makohozi kutoka katika zahanati na vituo vya afya ili kupelekwa katika hospitali kubwa kwa vipimo vya ugonjwa wa kifua kikuu.
Aidha imezindua dawa ya kutibu kifua kikuu kwa mara ya kwanza kwa ajili ya watoto wadogo nchini, jambo litakalosaidia kuepuka kutumia dawa ya watu wazima, jambo litakalopunguza matokeo hasi ya ugonjwa huo. Mtoto atakayekuwa na kilogramu 25 na zaidi atahitajika kupatiwa dawa ya watu wazima.
Kadhalika, imesema hairuhusiwi wanafunzi wanaokwenda shule za bweni kuingia bila kupimwa ugonjwa wa kifua kikuu na kuwaagiza waganga wakuu wa vituo vya afya na hospitali kutizama hilo.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe Ummy Mwalimu alisema hayo jana Dar es Salaam wakati akizindua dawa hiyo ya watoto pamoja na kukabidhi mashine maalumu tano zinazogharimu Sh milioni 170 kwa hospitali binafsi kwa ajili ya kusaidia kupima ili kupambana na Kifua Kikuu.
Hospitali zilizokabidhiwa mashine ili kujikita katika kupambana kutokomeza ugonjwa wa kifua kikuu ni Hindul Mandal, Aga Khan, Regency, Kairuki na TMJ. Machi 24 ya kila mwaka ni Maadhimisho ya Kifua Kikuu Duniani. Kuhusu sampuli za kifua kikuu, Waziri Ummy alisema katika kuhakikisha serikali inapambana na ugonjwa wa kifua kikuu, ilielekeza hospitali kupima na huduma ziweze kupatikana kuanzia ngazi ya chini.
“Ili kuweza kutekeleza hilo, tunafikiria kushirikiana na bodaboda na kuingia nao mikataba ili wasafirishe sampuli ya makohozi kutoka ngazi ya chini na kupeleka hospitali kubwa na watalipwa,” alisema Waziri Ummy bila kufafanua zaidi mpango huo utafikiwa na kutekelezwa rasmi lini.
Kuhusu dawa ya watoto alisema katika wagonjwa 160,000 wanaougua ugonjwa huo nchini kwa mwaka, miongoni mwao watoto ni 6447 ikiwa ni sawa na asilimia 10 na ambao hufariki dunia ni wengi kutokana na kutojulikanika, kuchelewa kupatiwa huduma na hata kutogundulika mapema.
Alisema pamoja na kuwepo kwa idadi hiyo ya wagonjwa, lakini dawa walizokuwa wakitumia ni dawa za watu wazima, jambo ambalo lilikuwa ni changamoto kubwa. Alisema kuanzia Desemba 2015 Shirika la Afya Dunia (WHO) kwa kushirikiana na wadau mbalimbali walianzisha dawa za watoto aina ya mseto ulioboreshwa ambazo huyeyuka vizuri, ikiwa na ladha nzuri hazikatwikatwi.
“Dawa hizo tayari zimewasili na serikali imeanza kuzisambaza nchini kote katika vituo vya afya na kuwasihi watumishi wa sekta ya afya kuhakikisha inatoa dawa sahihi kwa watoto kulingana na maelekezo,” alisema Mhe Ummy na kuongeza kuwa kwa watoto wenye kilogramu zaidi ya 25 ndio pekee watakaopatiwa dawa za watu wazima.
Alizitaja baadhi ya dalili ambazo mtoto anazokuwa nazo ni mtoto kuwa na homa za mara kwa mara, kupungua uzito, kulialia, kikohozi kisichopungua, kutokuchangamka wala kupenda kucheza na hata homa za usiku.
Kuhusu wanafunzi wa bweni alisema ugonjwa kifua kikuu upo kila eneo na zaidi katika mazingira ambayo kila mmoja anaishi. Kuhusu ugonjwa wa kifua kikuu nchini alisema kwa Tanzania vifo vitokanavyo na ugonjwa huo ni 28,000 kwa mwaka ikiwa na maana kuwa kila siku hufa watu 77 na makadirio katika ugonjwa kwa mujibu wa takwimu za mwaka 2016 watu 160,000 huugua kila mwaka kati yao 65,900 ndio pekee wanaofikiwa na kuwekwa katika mpango maalum wa matibabu huku asilimia 60 wakibakia.
Alisema changamoto kubwa ni kupatikana kwa wanaoumwa na kuingizwa katika matibabu ambapo takriban wagonjwa 94,000 hawawezi kufikiwa hivyo kushindwa kugundulika.
Tanzania ni moja ya nchi 30 duniani yenye maambukizi. Ummy alisema mpango mwingine ni kushirikisha sekta binafsi, vituo vya afya vya umma katika kupambana na ugonjwa huo na asilimia 15 ya vituo binafsi vilikubali kutoa huduma na tiba katika mwaka 2014 asilimia 5.5 ya wagonjwa walibainika na baada ya mpango huo vituo hivyo viliweza kubaini asilimia 10.4.
Alisema hatua nyiongine iliyotumiwa katika ugunduzi wa ugonjwa huo ni kutumika kwa mashine maalumu 189 zilizogawanywa katika vituo vya afya zenye kupima kwa haraka zaidi na kutoa majibu ndani ya saa mbili badala ya saa 24 a mbapo vipimo hivyo ni bure.

No comments:
Post a Comment