Askari wa usalama barabarani amegongwa na gari kwenye Mataa. - KULUNZI FIKRA

Friday, 16 March 2018

Askari wa usalama barabarani amegongwa na gari kwenye Mataa.

Ofisa wa Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani ambaye Jina lake halijatajwa amepata ajali ya kugongwa na gari wakati akiongoza magari katika makutano ya Barabara yaliyopo Kijitonyama maarufu kama Mataa ya Sayansi jijini Dar es salaam.

Hayo yamesemwa Leo Machi 16, 2018 na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar, Lazaro Mambosasa wakati akizungumza na wanahabari jijini humo.

“Hii ni taarifa ya kusikitisha kuhusu ofisa wa Jeshi la polisi aliyekuwa kazini akiongoza magari pale Mataa ya Sayansi, amegongwa na gari na madereva wasiozingatia sheria za usalama barabarani, amevunjika mkono kwenye kiwiko na juu ya kiwiko, pia ameumia kichjwa kwani alianguka chali", alisema kamanda Mambosasa.

 “Muda mfupi uliopita nimetoka kumuona hospitali anaendelea vizuri. Niwaombe madereva wazingatie sheria za barabarani",alisema kamanda Mambosasa.

"Bila askari wa usalama barabarani tutashindwa kwenda makazini na walioko makazini watashindwa kurudi nyumbani,” alisema kamanda Mambosasa.

No comments:

Post a Comment

Popular