Waziri Kigwangalla : kuna gazeti limenichafua kuwa nimepingana na agizo la Rais Magufuli. - KULUNZI FIKRA

Wednesday, 1 November 2017

Waziri Kigwangalla : kuna gazeti limenichafua kuwa nimepingana na agizo la Rais Magufuli.

 
 Kuna chombo kimoja cha habari kimenichafua, kuwa nimepingana na agizo la Mhe. Rais kwa kuruhusu mifugo iingizwe ndani ya Hifadhi zote za Taifa, ikiwemo Serengeti. Jambo ambalo sikulisema.

Najua lengo ni kunichonganisha na Mamlaka iliyoniteua. Najua watu wa aina hii watakuwa wengi sana kwa sasa sababu nimegusa maslahi ya watu wengi sana kwa maamuzi magumu niliyofanya siku za karibuni, kuanzia kwenye suala la kufuta mchakato wa vibali vya uwindaji, kupambana na majangili hadi kuanza mchakato wa kurudisha kwenye umiliki wa Serikali hoteli zote zilizokuwa za Serikali kupitia Shirika letu la Tanzania Tourist Corporation kwa kushindwa kwao kuziendeleza kwa tija kwenye sekta ya Utalii.

Mimi nilistisha Operesheni iliyoendeshwa kwenye eneo la km 5 nje ya mpaka wa Serengeti ndani ya Pori la Tengefu la Loliondo kwenye ardhi yeye mgogoro, na ni baada kupokea taarifa za ukiukwaji wa sheria za vijiji, na uwepo wa minong'ono kwamba Serikali iliendesha Operesheni hiyo kwa kutekeleza matakwa ya muwekezaji.

Jambo nililoona linaichafua Serikali na Mhe. Rais. Nilifanya hivyo sababu najua kuna kamati ya Mhe. Waziri Mkuu inashughulikia suala la mgogoro wa Pori la Tengefu la Loliondo.

Sikuona sababu ya kuanzisha operesheni wakati bado kuna uamuzi wa suluhu ya mgogoro ipo mezani kwa Mhe. Waziri Mkuu binafsi.

Binafsi nimekisamehe chombo hiki, lakini ili wajifunze kuwa mimi si mtu wa kuchezea waombe radhi haraka kabla sijawaburuza kwa Waziri wa Habari, Dr. Mwakyembe, nikiwa na ushahidi wangu ili achukue hatua stahiki.

No comments:

Post a Comment

Popular