UVCCM kwazidi kuwaka moto waraka mzito watolewa. - KULUNZI FIKRA

Tuesday, 14 November 2017

UVCCM kwazidi kuwaka moto waraka mzito watolewa.

 Mwaka huu (mwezi December) ni muhimu sana kwa Jumuiya ya Vijana ya CCM (UVCCM). Ni mwezi ambao Jumuiya linaenda kwenye uchaguzi ngazi ya Taifa kwa mara nyingine tena kwa kuwachagua viongozi wakuu akiwemo Mwenyekiti wa Jumuiya kurithi mikoba ya Ndugu. Sadifa

Lazima tukiri wazi ya kwamba zaidi ya miaka 10 uongozi wa Taifa UVCCM haujakidhi mahitaji na matakwa ya vijana nchini. Nitakuwa sijawatendea haki vijana wenzangu kama sitasema wazi hapa kwamba uongozi huu unaomaliza muda wake chini ya Sadifa ndio umekuwa uongozi mmbovu kuwahi kutokea ndani ya Jumuiya yetu. Hili halipo machoni mwa vijana wengi nchini hata Mh. Rais wetu mpendwa Magufuli aliliona hili na kuyasena wazi wazi akiwa katika kongamano la vijana wa Shirikisho Kigamboni.

Uchaguzi wa mwaka huu 2017 ni muhimu sana kwetu hata kama viongozi tunaoenda kuwachagua wanajitambua ama hawajitambui. Muhimu ni kwamba muelekeo wa Jumuiya yetu utategemea sana maamuzi yetu. Ni dhahiri hii miaka 5 tumekuwa mashahidi wa namna Jumuiya yetu imekuwa ya ovyo. Jumuiya yetu kwa sasa inachangamoto nyingi ambazo zinahitaji akili za pamoja kuzitatua, na katika msingi huo tunahitaji Mwenyekiti atakayeleta vijana wote kwa pamoja kutatua changamoto hizo.

*Tunahitaji Mwenyekiti mwenye uwezo. Tunahitaji Mwenyekiti msomi. Tunahitaji Mwenyekiti imara. Tunahitaji Mwenyekiti mwenye upeo mpana. Na kubwa, Tunahitaji kuwa organized zaidi ili kutatua changamoto zinazotukabili vijana kwa pamoja*.

*Tunahitaji Mwenyekiti ambaye ataamsha hisia za vijana kuhusu Jumuiya, kuhusu utaifa na kuhusu uzalendo na kuhamasisha vijana kufanya kazi kwa manufaa ya Taifa na serikali ya awamu ya tano*.

Wengi wamejitokeza kuomba ridhaa katika nafasi hiyo ya juu, hatua ambayo tafsiri yake ni ukuaji wa demokrasia katika awamu hii, ingawa ukweli ni kwamba ni wachache sana wenye uwezo wa kushika nafasi hiyo. Kama vijana tuna imani kubwa sana na vikao vya Chama vitakavyofanyika hapa karibuni, tuna imani kubwa sana sana na Mwenyekiti wetu wa Chama na kwa kuwa kwake kipaumbele katika utendaji ni Uwezo wa mtu basi niwatoe hofu vijana wenzangu kuwa safari hii tutaletewa wagombea wenye uwezo na kisha tutapata Mwenyekiti bora na mwenye uwezo. Na mwenye dira ya kututoa hapa tulipozamishwa na huu uongozi wa sasa...

Kuna baadhi ya viongozi wa sasa (Mawaziri, Manaibu waziri, RC's) wenye wagombea wao tayari ila niweke wazi tu kwamba watusamehe, kwa sasa ni lazima tujenge Jumuiya yetu ambalo litatumikia vijana wote nchini na sio kutumikia baadhi ya viongozi. Uchaguzi wa 2008 tulishuhudia Jumuiya ikitumika. 2012 mpaka sasa tumeendelea kushuhudia Jumuiya ikitumiwa ovyo na baadhi ya wanasiasa. Sasa 2017 tunasema hapana Jumuiya yetu iachwe huru ili kiitumikie vijana nchini kwa kuhamasisha maendeleo.

Rais Magufuli amefanya na anaendelea kufanya kazi kubwa sana sana inayohitaji pongezi za dhati, hivyo ili kumsaidia ni lazima Jumuiya iachwe huru na wanasiasa wanaopandikiza watu wao wakiwemo viongozi wa sasa wa Jumuiya..

UVCCM inahitaji mabadiliko makubwa ya kimuundo, kifikra na kimfumo. Hatuwezi tena kukubali kukaa miaka 5 mingine bila kuendelea mbele. Kuna nafasi kubwa sana kwetu vijana kuendelea zaidi ya tulipo sasa na hili litatokea tu, kama tukipata kiongozi sahihi, imara, mwenye uwezo, msomi na kubwa zaidi kama tukisikilizana na kuwa na sauti moja.

Ni jukumu letu vijana kusimama na kutembea kifua mbele kwa kumsapoti Rais wetu Magufuli na kutokana na sababu hizo vijana hatuna budi kuliomba vikao husika vya Chama kupitia wasifu wa kila mgombea na kisha kutuletea watu sahihi na wenye uwezo...

No comments:

Post a Comment

Popular