Tanesco imebomoa nyumba zaidi ya 200 zilizo chini ya umeme mkubwa. - KULUNZI FIKRA

Thursday, 16 November 2017

Tanesco imebomoa nyumba zaidi ya 200 zilizo chini ya umeme mkubwa.

 Zaidi ya nyumba miambili zimebomolewa zilizopo karibu na umeme mkubwa wa TANESCO katika eneo la Mabibo hadi bonde la Msimbazi na kuziacha familia bila ya makazi hali iiliyosababisha vitendo vya wizi na uharibifu wa mali zikiwemo Samani,Magodoro pamoja na vifaa mbalimbali

Kulunzifikra blog imefika katika tukio hilo la bomoabomoa na kukuta watu wakiangaika kuokoa baadhi ya mali huku wengine wakiwa na nyuso za kukata tamaa baada ya mali zao kufunikwa matofali, wengine wakilalamikia vitendo vya wizi unaofanywa na baadhi ya vijana katika eneo hilo.

Wakati hao wakilalamikia upotevu wa mali zao  kulunzifikra blog imeshuhudia baadhi ya wananchi wakiangaika kubomoa wenyewe nyumba zao kwa lengo la kuokoa mabati na vifaa vingine vya ujenzi, huku wengine wakihamisha vitanda, magodoro ambapo wakizungumza na waandishi wa habari wamesema licha ya kuwekewa alama ya x kwenye hizo nyumba lakini kesi ili kuwa mahakamani hivyo wangepewa taarifa ili waweze kuondoa mali zao.

Kulunzifikra blog  imemtafuta msemaji wa shirika la umeme nchini ili kuzungumzia swala hilo ambapo ametoa taarifa kuwa yuko katika kikao, ambapo kumbukumbu zinaonyesha kuwa nyumba hizo ziliwekwa alama ya x muda mrefu na wakazi hao walitakiwa kubomoa nyumba wenyewe na kuondoka katika maeneo hayo hatarishi yanaliyo chini ya umeme mkubwa wa TANESCO ambayo kwa mujibu wa sheria yanamilikiwa na shirika la umeme nchini TANESCO, jambo ambalo walipinga na kuamua kwenda mahakamani.

No comments:

Post a Comment

Popular