Waziri wa Fedha wa utawala uliopita wa rais mstaafu Jakaya Kikwete, Saada Mkuya amemshukia Waziri wa Fedha, Dk Philip Mpango kwa kuandaa mpango wa taifa wa maendeleo pasina kuihusisha Zanzibar.
Mkuya ambaye ni mbunge wa Welezo visiwani Zanzibar amesema, Dk Mpango amekuwa na kawaida ya kutojibu hoja ambazo zinatolewa na wabunge wa Zanzibar jambo ambalo imemsikitisha.
Akichangia leo Novemba 10 bungeni mjini Dodoma Mpango wa Maendeleo ya Taifa, Mkuya
ambaye katika mchango wake alizungumzia kusikitishwa kwake na jinsi Waziri Mpango anavyoitenga Zanzibar licha ya kuwa ni sehemu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
“Nadhani taifa hili la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania linaundwa na pande mbili sasa
Mwenyekiti (Azzan Zungu) cha kusikitisha na fedheha kabisa ni kuona hakuna hata
eneo moja lililopangiwa mpango angalau tu likaelekezwa katika upande mwingine wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,” alisema Mkuya.
“Hili niliseme wazi mheshimiwa mwenyekiti kupitia kwako, mheshimiwa Waziri wa Fedha (Dk Mpango) wakati tunajadili bajeti Juni mwaka huu baadhi ya wenzangu tunaotoka upande wa pili wa Muungano tulichangia maeneo fulani fulani,” ameongeza
Mkuya
‘’Lakini kwa masikitiko makubwa mheshimiwa mwenyekiti hakuna eneo hata moja lililoguswa likajibiwa hoja angalau kule upande wa pili wakasikia na mimi nilichukua hatua kwenda kumuuliza mheshimiwa waziri wa fedha mbona angalau hata hoja mbili ili nao waone ni sehemu ya muungano.”
“Kuna masuala mengine hayahitaji lazima iwe ni wizara inayoshughulika na Muungano, kuna
mambo mengine ishu zingine zinahitaji ‘coordination’ za pande mbili hivi kweli kama hii ya utalii kunaweza kuwa na project bila kuihusisha Zanzibar haipo?

No comments:
Post a Comment