Prof Kitila jino kwa jino na Lazaro Nyalandu katika uchaguzi. - KULUNZI FIKRA

Friday, 17 November 2017

Prof Kitila jino kwa jino na Lazaro Nyalandu katika uchaguzi.

 
Hayawi hayawi, sasa yamekuwa. Kile kitendawili kigumu kilichokuwa kimekosa majibu sasa majawabu yake yako bayana! Kuna kila aina ya dalili CCM wanamuandaa Prof Kitila Mkumbo kuchauana vikali na Ndugu Lazaro Nyalandu katika uchaguzi mdogo unaotarajiwa kufanyika kumchagua mbunge wa Jimbo la Singida Kaskazini baada ya Ndugu  Nyalandu kujiondoa CCM na kujiunga CHADEMA hivi karibuni.

Wataalamu wa masuala ya siasa wanabainisha kuwa CCM wamejithathmini na kuona wamteue Prof Kitila kuwa mgombea wao ili achuane na mgombea wa upinzani, Ndugu Nyalandu.

Sababu zinazopelekea CCM walenge kumteua Prof Kitila ni kutokana na hali ya siasa za Kanda ya Kati ambazo hazitabiriki hata kidogo. Inadhaniwa Prof Kitila ana uwezekano wa kumuangusha Dr Nyalandu katika uchaguzi huo kwa kuwa bado ana chembechembe za upinzani, hivyo kuweza kujizolea mashabiki kutoka upande wa upinzani pamwe na upande wa CCM.

Aidha,upande wa CHADEMA nao wanatamba kuibuka washindi katika jimbo hilo kutokana na kuwa na hazina nzuri ya wafuasi, huku wakitarajia kupata "kura za chuki" za kutosha kutoka kwa wanaCCM, hasa wale wanaokerwa jinsi nchi inavyotawaliwa kwa sasa.

No comments:

Post a Comment

Popular