Nape Nnauye aikosoa serikali kuhusu hali ya uchumi nchini. - KULUNZI FIKRA

Saturday, 11 November 2017

Nape Nnauye aikosoa serikali kuhusu hali ya uchumi nchini.

Mbunge wa Mtama Mhe Nape Nnauye amedai kwamba ameshtushwa sana na mapendekezo ya serikali kuhusu kuwekeza pesa kwenye miradi ambayo inaweza kuendeshwa kibiashara.
Akichangia leo Bungeni kwenye mjadala wa kujadili Mpango wa Taifa , Mhe Nape amesema kwamba baadhi ya miradi ambayo ingeweza kutekelezwa na sekta binafsi ni ujenzi wa reli ya kisasa ya kati, mradi wa umeme Rufiji, mradi wa bandari na uboreshaji shirika la ndege.
Nape amesema kwamba aliposoma mapendekezo alishtuka baada ya kuona kwamba Serikali inapendekeza kuwekeza pesa za Serikali kwenye miradi ambayo inaweza kuendeshwa kibiashara ambayo pia watu binafsi wangeruhusiwa kuiendesha.

"Kama mpango huu utatekelezwa kama ulivyo, miradi hii inakwenda kuuwa uchumi wa nchi yetu. Miradi hii mikubwa inaweza kujiendesha kibiashara na ikajilipa yenyewe, Niweke rekodi sawa Sipingi kutekelezwa kwa miradi   mikubwa ila napingana na Serikali jinsi ya kuifadhili na kuiendesha kwa kutumia fedha za Serikali"amesema Mhe Nape.

Akiendelea kusimamia hoja yake Mh. Nape amesema kuwa miradi hiyo ni mikubwa na itagharimu fedha nyingi ambazo zitailazimisha Serikali kukopa fedha nyingi, hali ambayo itaathiri deni la taifa ambalo kwa sasa Dola bilioni 26.

“Serikali ikienda kukopa na kwa sababu miradi hii inachukua muda mrefu maana yake tutaanza kulipa deni kabla ya miradi hiyo haijaanza kurudisha faida kwa taifa. Kwanini tunataka kung’ang’aniza kuchukua pesa ya Serikali”. Hebu tufikirie upya. Dkt Mpango rudini mkafikiri upya” amesema Mhe  Nape.

Nape ameongeza kwamba "Huu mpango wako mzuri lakini rudini kwenye mawazo ya kutumia sekta binafsi. Tukienda hivi tunaenda kuua uchumi,”alisema Mhe Nape.

No comments:

Post a Comment

Popular