Mbunge wa Chadema amshukuru spika Ndugai kwa kumlinda. - KULUNZI FIKRA

Friday, 17 November 2017

Mbunge wa Chadema amshukuru spika Ndugai kwa kumlinda.

 
 Mbunge wa Tarime Vijijini, Mhe John Heche amekiri bila busara za Spika wa Bunge kutumika leo angekuwa amekamatwa leo na polisi wamedaiwa kutoka Morogoro waliokuwa eneo la Bunge kwa nia ya kumkamata.

Mhe Heche amweka hilo wazi jioni ya jana  huku akikosoa matumizi mabaya ya rasilimali iliyotumiwa.

"Nimepokea barua ya polisi asubuhi leo wakinitaka kuripoti Morogoro eti kwa kosa la kumsindikiza na kufanya mkutano jimboni kwa Mh Lijualikali alipotoka gerezani mwezi wa nne"  alisema Mhe Heche.

Ameongeza kwamba "Kabla hata ya kuitikia wanataka kunikamata bila busara za spika wangenikata. Matumizi mabovu ya rasilimali"
Kabla ya taarifa hii kutoka Mapema Jana Mhe  Heche alikiri kupokea wito unaomtaka kwenda kuhojiwa Morogoro.

"Nimepewa wito kuwa natakiwa nikahojiwe Morogoro. Nimepokea wito huu na tayari nao wako hapa. Siamini kama Spika ataruhusu hili," amesema Mhe Heche.

No comments:

Post a Comment

Popular