Lowassa amuomba Rais Magufuli kuwa msikivu kwa watu wanaotoa maoni yao. - KULUNZI FIKRA

Tuesday, 14 November 2017

Lowassa amuomba Rais Magufuli kuwa msikivu kwa watu wanaotoa maoni yao.

 
 Waziri Mkuu wa zamani na mjumbe wa Kamati kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Ndugu Edward Lowassa amemuomba Rais Dkt. John Magufuli kusikiliza maoni ya watu wengi ambayo wanataka kuendelea kwa mchakato wa katiba kabla ya kufanyia maamuzi ya kuachana na suala hilo.

Katika ufunguzi wa kampeni za udiwani kwenye Kata ya Moita wilayanI Monduli ambao ulihudhuriwa na waziri mkuu huyo wa zamani Ndugu Edward Lowassa ambaye ametumia jukwaa hili kutoa rai kwa rais Magufuli kusikiliza wanaotaka mchakato huo uendelee.

Katika hoja zake za kwa nini mchakato wa Katiba uendelee, Ndugu Lowassa amesema yapo masuala ya msingi ikiwemo muungano wa vyama katika kuendesha serikali kulingana na matokeo yanayopatikana katika uchaguzi pamoja na uanzishwaji holela wa vyama vya siasa ambavyo wakati mwingine hutumiwa na vyama vingine wakati wa uchaguzi.

Mbele ya wakazi wa Kata ya Moita ambayo inajiandaa na uchaguzi wa marudio, Loburu Lomnyaki Kivuyo ndiye anayepeperusha bendera ya CHADEMA, anasema atahakikisha elimu ya watoto wa wafugaji hao anaisimamia ipasavyo huku baadhi ya viongozi wa chama hicho wakimnadi mgombea wao.

No comments:

Post a Comment

Popular