Nimepata taarifa kwamba ninatafutwa na Jeshi la Polisi Arusha kwa maelekezo kutoka juu. Ninaelezwa kuwa mipango mingi inapangwa juu ya uchaguzi wa marudio hapa Arusha , tunatarajia kuwa na wakati mgumu sana ktk kampeni hizi, na hivi sasa tunaanza kushuudia mateso ya aina mbali mbali.
Watesi wetu wanapata sifa na vyeo kwa namna ya ukatili wanaonyesha dhidi yetu , kila wakati tulipolalamika dhidi ya matendo mabaya na nia ovu , tulifikiri tunafanya jambo jema na muhimu , lakini badala yake uovu wao umekuwa msaada ktk kazi zao . Wengine wamepanda vyeo kwa sababu ya ukatili , kukandamiza haki na demokrasia , tunarudi kwenye uchaguzi leo kwa sababu pia ya rushwa , hata walitoa rushwa hadharani walipandishwa cheo badala ya kukutana na mkono wa sheria.
Ni dhahiri sasa Dc anayetaka kuwa RC ni lazima awe na tabia na matendo ya aina hii , hali kadhalika kwa nafasi nyingine mbali mbali. Hili ni tishio kubwa la usalama wa Nchi yetu.
Hakuna majadiliano ya kikazi kati ya Viongozi wa upinzani na Serikali , kwani hali yoyote yakuonyesha mahusiano mema kati yetu na Viongozi wa Serikali ni risk kwa kazi zao. Kwa hiyo namna pekee ya wao kuonyesha nidhamu na utendaji uliotukuka kwa Mamlaka zao za uteuzi ni kuonyesha na kutenda mahusiano na matendo mabaya dhidi yetu.
Ubaguzi huu unakua kwa kasi sana , hii ni saratani , wako wengi wanaotuonea huruma na wachache hawataelewa msingi huu wa malalamiko yetu , wanafikiri msalaba huu unatustahili sisi peke yetu kumbe ni msalaba wetu sote kama Taifa.
Wachache hao walioko mahabusu kifikra wanahitaji msamaha wetu .
Martin Luthet Jr alipata kusema " Injustice anywhere is threat to justice everywhere " akaendelea kusema " Whatever affects one directly , affects all indirectly .
Tusikate tamaa , baada ya giza nene asubuhi utokea .
Godbless J Lema (MB)

No comments:
Post a Comment