Geita : Mwanafunzi wa darasa la tano amejifungua mtoto katika choo cha shule. - KULUNZI FIKRA

Wednesday, 8 November 2017

Geita : Mwanafunzi wa darasa la tano amejifungua mtoto katika choo cha shule.

 Katika hali ya isiyo ya kawaida, mwanafunzi wa darasa la tano katika shule ya Msingi Ibondo, Kata ya Rudete, Wilayani Geita, mwenye umri wa miaka 13 amejifungua kabla ya wakati katika choo cha shule baada ya kupata uchungu wa ghafla.

Hali hiyo imezua taharuki miongoni mwa wanafunzi na walimu shuleni hapo ambapo mwanafunzi huyo alikimbilia chooni baada ya kujisikia haja kubwa na badala yake alitoka mtoto wa umri wa miezi minne.

Akisimulia mkasa mzima, mwanafunzi huyo ambaye amelazwa katika zahanati ya Ibondo kwa matibabu zaidi, amesema muhusika wa ujauzito huo ni kijana mkaazi wa kijiji cha Ibondo ajulikanaye kwa jina la Laurent Ngasa.

Amesema awali alikuwa akijisikia vibaya tangu asubuhi ambapo alipata maumivu ya kichwa, na baadaye wakati wa masomo alijisikia kupata haja kubwa na ndipo alipokwenda chooni kwa nia ya kujisaidia.

Amekiri kwamba alikuwa na ujauzito uliokuwa na muda wa miezi minne, lakini hakuwahi kuwashirikisha wazazi wala walimu wake.

Inadaiwa kuwa walimu walianza kumhisi mwanafunzi huyo kuwa na ujauzito siku ya ijumaa iliyopita,lakini kabla hawajachukua hatua yoyote ndipo mwanafunzi huyo akawa amejifungua.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka katika zahanati ya kijiji hicho, wahudumu walifanikiwa kumfanyia vipimo na kujidhihirisha kuwa ni ujauazito na wakampatia huduma.

Akifafanua juu ya hali ya usalama wa mtoto huyo, muhudumu wa Zahanati ya Ibondo, Aloyce Aron, amesema walimpokea mtoto huyo saa 7.30 mchana ambapo vipimo vilionyesha kuwa alikuwa na mimba ya umri kati ya miezi minne.

No comments:

Post a Comment

Popular