CCM Singida : Lazaro Nyalandu alishinda ubunge kwa rushwa. - KULUNZI FIKRA

Friday, 3 November 2017

CCM Singida : Lazaro Nyalandu alishinda ubunge kwa rushwa.

 Mwenyekiti Wa CCM Mkoa Wa Singida, Martha Mlata Amesema Kuwa Lazaro Nyalandu Alianza Kuwa Shida Tangu Alipoteuliwa Kuwa Naibu Waziri Wa Viwanda Na Biashara, Aliposhindwa Kufanya Kazi Za Ubunge Jimboni Kwake.

"Kwa Hiyo Akawa Mzigo Jimboni Kutokana Na Kutofika Na Akifika, Anasimama Jukwaani Dakika Mbili Halafu Anashuka Huku Kukiwa Hakuna Cha Maana Alichokiongea. Na Hata Alipokuwa Jimboni, Hakuweza Kuwatetea Wananchi Wake Na Hatimaye Akawa Bubu Kabisa" - Mlata.

Mlata Alidai Kuwa Katika Kipindi Chote Cha Ubunge, Nyalandu Hakuwahi Kushinda Kwa Kupigiwa Kura Na Wananchi Zaidi Ya Kuhonga Wapiga Kura Na Shughuli Zote Za Ubunge Zilikuwa Zikifanywa Na Wasaidizi Wake Watatu Na Yeye Anafika Jimboni Ikiwa Zimebaki Siku Saba Za Uchaguzi.

No comments:

Post a Comment

Popular