Bodi ya mikopo imesema hakuna mwanafunzi ambaye atapata mkopo wakati hana vigezo. - KULUNZI FIKRA

Tuesday, 7 November 2017

Bodi ya mikopo imesema hakuna mwanafunzi ambaye atapata mkopo wakati hana vigezo.

 
  Bodi ya mikopo ya elimu ya juu HESLB imesema hakuna mwanafunzi ambaye atapata mkopo wakati hana vigezo stahiki ambavyo vimeainishwa.

Hayo yamebainishwa leo na Mkurugenzi wa bodi hiyo Abdul Razaq Badru baada ya kuwepo kwa mkanganyiko wa wanafunzi wa mwaka wa kwanza waliokosa mkopo.

“Waombaji waliofika ofisini na wale ambao hawajafika tumesikia malalamiko yao na tunayafanyia kazi lakini mikopo watapata wenye sifa pekee kama huna sifa huwezi kupata mkopo”, amesema Badru.

Aidha Mkurugenzi amesema bajeti ya fedha za mikopo kwa mwaka wa masomo wa 2017/18 ni bilioni 427, kwaajili ya wanafunzi 122,000 wakiwemo wa mwaka wa pili na watatu, huku zaidi ya wanafunzi elfu 30 wa mwaka wa kwanza wakiwa kwenye bajeti ya kupata mkopo.

Badru amesema hadi saa wanafunzi 29,578 tayari wameshapata mikopo kiasi cha shilingi bilioni 96 na wameshaaanza masomo kwasababu walitimiza sifa za kupata mkopo. Amesisitiza kuwa hakuna mwanafunzi atakayekosa mkopo wakati amekidhi vigezo na sifa za kupata mkopo.

No comments:

Post a Comment

Popular