Mapato ya Serikali Kwa miezi ya Julai na Agosti yameshuka mpaka chini ya Shilingi 600 bilioni. Ni mporomoko mkubwa Sana na sio jambo la kushangilia hata kidogo. Madhara ya kushuka Kwa mapato ni makubwa kwani Mishahara ya Watumishi wa Umma peke yake ni Shilingi 570 bilioni Kwa Mwezi. Kwanini mapato yanashuka?
Mzee Harry Kitilya alipata kuniambia mwaka 2013 " Mwenyekiti, TRA inatoza kodi kutoka kwenye shughuli za Biashara zinazozalisha Mapato na sio kutoka kwenye Biashara tu ". Kitilya alikuwa na maana kuwa Kama hakuna shughuli za biashara ( business transactions), huwezi kutoza kodi. Maelezo haya yanaeleza kwanini Mapato ya Serikali yameshuka. Shughuli za Biashara zimeshuka sana nchini na hivyo kupelekea kuporomoka Kwa mapato.
Kodi inayoingiza mapato mengi Serikalini ni PAYE ( kutoka mishahara ya wafanyakazi). Kitabu cha Mapato ya Serikali Kuu cha mwaka 2016/17 kinaonyesha kuwa Wafanyakazi wote wa sekta ya Umma na Sekta Binafsi walichangia jumla ya shilingi trilioni 3 kwenye mapato yote ya Serikali. Hivi karibuni tumeshuhudia makampuni yakipunguza wafanyakazi na mengine kufungwa. Pia Serikali yenyewe ilipunguza watumishi iliyowaita hewa na wenye vyeti feki. Hivyo eneo kubwa la kodi ya PAYE limeathirika.
Serikali inapaswa kutazama upya utendaji wake ili kuweka mazingira mazuri ya biashara na uwekezaji. Vinginevyo Serikali itabidi kukopa ili kulipa mishahara.
Saturday, 7 October 2017
Home
Unlabelled
Zitto kabwe: Mapato ya serikali yameporomoka mpaka chini ya shilingi bilioni 600
Zitto kabwe: Mapato ya serikali yameporomoka mpaka chini ya shilingi bilioni 600
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Popular
-
THIS ANNOUNCEMENT CONTAINS INSIDE INFORMATION Acacia Mining plc (“Acacia” or the “Company” or the “Group”) Management Changes Ac...
-
Tanzania’s Tunduru district is a major producer of gem-quality sapphire and ruby, along with exotic gems such as alexandrite and tsavor...
-
Moto mkubwa umelipuka na kuunguza soko la wafanyabiashara wadogo wadogo (machinga) katika eneo la Mbagala Rangi Tatu – Dar, asubuhi hii M...
-
Ofisi ya Spika wa Bunge imesema, mpaka sasa haijapokea barua toka kwa aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Singida Kaskazini kupitia Chama cha...
-
Spika wa zamani, Pius Msekwa amesema Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu hakuwa analazimika kuandika barua kwa Spika wa Bunge...

No comments:
Post a Comment