Wenda Kenya ikaingia kwenye mgogoro wa kuwa na marais wawili - KULUNZI FIKRA

Sunday, 29 October 2017

Wenda Kenya ikaingia kwenye mgogoro wa kuwa na marais wawili

Wenda nchi ya Kenya ikakumbwa na mzozo mkubwa wa kisasa mwaka huu iwapo Rais Uhuru Kenyatta anayeongoza katika kura ambazo zinazozidi kutolewa na tume ya uchaguzi IEBC kama atatangazwa mshindi na kuapishwa.

 Baadhi ya viongozi wa muungano wa upinzani NASA nchini Kenya, wamesema jana Jumamosi kwamba iwapo Rais Uhuru Kenyatta atalishwa kiapo cha muhula wa pili baada ya uchaguzi wa marudio wa nafasi ya urais uliozua utata, basi watamuapisha kiongozi wao Raila Odinga kama Rais.

 Wakizungumza katika eneo la Mavoko Kaunti ya Machakos, wanasiasa hao, wakiongozwa na wakili wa muungano huo na Seneta wa Kaunti ya Siaya, James Orengo, walisema kuwa watafanya uchaguzi mwingine chini ya kipindi cha siku 90.

  Aliyekuwa Seneta wa Machakos Johnston Muthama alisema Muungano huo uko tayari kumuapisha kiongozi wao.

 "Wakimuapisha Uhuru, nasi tutamuapisha Raila", Muthama aliuambia umati wa watu uliokusanyika mjini Mavoko.

  "Uchaguzi huru na wa haki ni lazima ufanyike ndani ya siku tisini",alisema Orengo.
    Haya yalijiri huku tume huru ya uchaguzi na mipaka IEBC, ikiendelea kujumulisha kura katika kituo cha Kitaifa cha Bomas of Kenya.
    

No comments:

Post a Comment

Popular