WAZIRI Nchi Ofi si ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Selemani Jaffo, amesifu mchango wa shule binafsi kwa juhudi kubwa wanazofanya katika kuiinua sekta ya elimu hapa nchini.
Jaffo alitoa sifa hizo jana wakati akifungua Mkutano Mkuu Maalumu wa siku moja wa Chama cha Wawekezaji Binafsi katika Elimu (TAPIE), uliofanyika Jijini Mwanza. Alisema mchango wa shule hizo umesaidia kuifanya Tanzania ionekane kuwa iko katika hali nzuri kielimu kwa kutoa vijana waliofuzu kimasomo na kuwa na uwezo kuiwakilisha katika mikutano mbalimbali ya nchi za nje.
Mkutano huo wa siku moja ulikuwa na lengo la kujadili namna ya kuboresha sekta ya elimu kwa kuwaleta pamoja wawekezaji na wamiliki wa shule binafsi kuwa na jukwaa la mijadala na midahalo kuhusu uendeshaji wa shule na maslahi ya jamii nzima.
Rais wa TAPIE, Ester Mahawe ambaye ni Mbunge wa Viti Maalumu, alisema serikali na wananchi kwa ujumla watambue taasisi hiyo ni chombo kinachowapatia fursa wamiliki kuwa sehemu ya uandaaji wa sera, miongozo na sheria za kuendeshea, kuwa kiungo muhimu na mshiriki wa kuisaidia serikali katika kuongeza fursa ya elimu kwa vijana wa Kitanzania na uboreshaji wa utoaji wa elimu hapa nchini.
“TAPIE inahakikisha maslahi ya wamiliki wa shule binafsi hapa nchini yanalindwa na kutetewa katika ngazi na idara zote za serikali na ikumbukwe changamoto za uwekezaji katika sekta ya elimu ni nyingi sana, kuanzia umiliki wa ardhi, kodi na tozo mbalimbali,” alisema.
Mahewa aliongeza kuwa Sheria na miongozo isiyo rafi ki kwa wamiliki, gharama za wafanyakazi, mikopo yenye riba kubwa ni changamoto, hivyo kwa sasa kinahitajika chombo chenye maono na dhamira ya dhati ili kuona mitaji na nguvu zinazotumika zinakuwa na tija na zinalindwa kimfumo.

No comments:
Post a Comment