Mtoto mwenye umri wa miezi kumi Arman Hassan Mohamedi, ameuawa na watu wasiojulikana katika eneo la Fuoni lililopo mkoa wa Mjini Magharibi Unguja visiwani Zanzibar, na kisha kumtumia ujumbe mama mzazi wa mtoto huyo.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kamanda wa Polisi mkoa wa Mjini Maghari Unguja, Hassan Nasir, amesema tukio hilo limetokea Oktoba 3, ambapo mtoto huyo aliuawa na kisha kutumbukizwa kwenye dumu la maji la lita 60, na kulitelekeza nyumbani kwao.
“Upelelezi wa awali unaonyesha aliuawa na mtu ambaye hajafahamika bado, tunasema ameuwawa kwa sababu alikuwa alikuwa nje na watoto wenzake wakicheza, baada ya muda akatoweka, akatafutwa sehemu mbali mbali hadi vituo vya polisi, lakini kwenye saa moja na nusu akaonekana akiwa kwenye dumu la maji la lita 60 akiwa ndani amekufa, lakini kuna message alitumiwa mama wa mtoto kwamba mtoto wako atapatikana akiwa maiti, na nyingine ikimpa pole kwa msiba”, amesema Kamanda Nassir.
Kamanda Nassir amesema Jeshi la polisi mkoani humo linaendelea kuchunguza kwa kufuatilia messgae hizo ili kuwabaini waliofanya mauaji hayo, aliyoyaita ya kikatili na kuwachukulia sheria stahiki.
Thursday, 5 October 2017
Home
Unlabelled
Watu wasiojulikana waendelea kufanya mauaji Zanzibar
Watu wasiojulikana waendelea kufanya mauaji Zanzibar
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Popular
-
THIS ANNOUNCEMENT CONTAINS INSIDE INFORMATION Acacia Mining plc (“Acacia” or the “Company” or the “Group”) Management Changes Ac...
-
Tanzania’s Tunduru district is a major producer of gem-quality sapphire and ruby, along with exotic gems such as alexandrite and tsavor...
-
Moto mkubwa umelipuka na kuunguza soko la wafanyabiashara wadogo wadogo (machinga) katika eneo la Mbagala Rangi Tatu – Dar, asubuhi hii M...
-
Ofisi ya Spika wa Bunge imesema, mpaka sasa haijapokea barua toka kwa aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Singida Kaskazini kupitia Chama cha...
-
Spika wa zamani, Pius Msekwa amesema Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu hakuwa analazimika kuandika barua kwa Spika wa Bunge...

No comments:
Post a Comment