Hatimaye Mhe Tundu Lissu ametoa kauli ya kwanza iliyorekodiwa na kuambatanishwa na picha zinazomuonyesha akiwa amekaa na mwenye tabasamu, huku sauti ukiwa imara.
Katika sauti hiyo iliyosambaa mitandaoni jana jioni, Mbunge huyo wa Singida mashariki aliyeshambuliwa kwa risasi takribani 30 septemba 7 mjini Dodoma, anajitambulisha na kuelezea jinsi watu walivyostushwa na tukio hilo na kuwashukuru kwa umoja wao.
" Watanzania wenzangu, Mimi Tundu Lissu. Nazungumza kutoka katika kitanda cha hospitali ya Nairobi nchini Kenya" amesema Tundu Lissu.
"Kwanza kabisa naomba nitoe shukrani zangu kwa Mwenyezi Mungu wetu wa mapenzi, Mungu wetu wa maisha, Mungu wetu wa uponyaji kwa kuniweka hai mpaka hapa nilipo.
Kama isingekuwa Mwenyezi Mungu, maisha yangu yangeishia Dodoma siku ile lakini mwenyezi Mungu, huyu wa uponyaji, alisema huyu hata kufa. Naomba nimshukuru kwa hilo". Amesema Tundu Lissu.
"Nafikiri sitakosea nikisema kuwa niko hai kwa sababu ya maombi ya Watanzania hasa". Amesema Tundu Lissu.
Amesema vyama vya kitaaluma kote duniani ambavyo vinaushirika na chama cha wanasheria Tanganyika (TLS) vimesaidia katika matibabu yake na kwamba amepata ujumbe wa kuungwa mkono kutoka mataifa ya Marekani, Uingereza, Australia, New Zealand, Ubelgiji, Ujerumani na Kenya.
"Lakini kuna kundi ambalo sijalisemea ambalo linahitaji kutajwa kipekee kabisa: Madaktari , Wauguzi na Wafanyakazi wa kawaida was hospitali ya Nairobi nchini Kenya, wa hospitali ya mkoa wa Dodoma pamoja na wafanyakazi wa tiba kutoka taasisi nyingine ambao kwa njia mbalimbali walishiriki kuniponya. Nawapa pongezi zangu za dhati kabisa". Amesema Tundu Lissu.

No comments:
Post a Comment