Wakati mbunge wa Singida mashariki Mhe Tundu Lissu ( Chadema) akitarajia kufanyiwa oparesheni ya 15 wiki hii , taarifa mpya ambazo kulunzifikra blog imezipata zinadai kuwa Mbunge huyo tayari ameanza mazoezi ya viungo .
Chanzo vya uhakika kutoka ndani ya hospitali ya Nairobi nchini Kenya alikolazwa Tundu Lissu kwa zaidi ya siku 40 sasa. Chanzo hivyo vimedokeza kuwa ndani ya siku NNE kuanzia sasa kuna uwezekano mbunge huyo akatoka hospitalini.
Mhe Tundu Lissu ambaye pia ni Rais wa chama cha mawakili Tanganyika (TLS) alishambuliwa kwa risasi na watu wasiojulikana septemba 7 mwaka huu nyumbani kwake mjini Dodoma alilokuwa anahudhuria vikao vya Bunge.
Chanzo hivyo vya habari vilivyozungumza na kulunzifikra blog kwa sharti la kutotajwa majina, vilielezea kuwa taarifa za kitabibu zilionyesha kuwa Mhe Tundu Lissu angetoka hospitalini oktoba 31 mwaka huu. Lakini kutokana na hali yake kuendelea kuimarika anaweza kuruhusiwa kabla ya muda huo.
" Taarifa za kitabibu zilikuwa zinaonyesha kwamba oktoba 31 mwaka huu, Tundu Lissu atoke hospitalini lakini recovering (namna alivyopata nafuu) yake imeonekana mapema. Juzi ( jumamosi na jumapili) Mhe Tundu Lissu alianza kutolewa nje akiwa kwenye wheel chair akiota jua....hivyo ndani ya siku nne kuanzia sasa atakuwa ametoka ." kilisema chanzo hicho cha habari.
Pamoja na taarifa hizo, haijajulikana endapo mwanasheria huyo mkuu wa chadema akitoka hospitalini ataendelea kubaki kenya au atarudi Tanzania.
Kulunzifikra blog ilipomtafuta mwenyekiti wa chadema Freeman Mbowe simu yake iliita bila kupokelewa na hata alipotumiwa ujumbe mfupi wa maneno hakujibu.
Ikumbukwe kuwa msemaji wa suala la Mhe Tundu Lissu tangu kushambuliwa kwake ni Mbowe hivyo hakuna kiongozi mwingine wa chadema Aliyekuwa tayari kuzungumza hali yake.
Hata hivyo tangu aliposhambuliwa zaidi ya siku 40 sasa hakuna mshiriki yoyote aliyekamatwa na kufikishwa mahakamani licha ya jeshi la polisi kutoa hadi za Mara kwa Mara kulishugulikia uchunguzi wa jambo hilo

No comments:
Post a Comment