Tatizo linalofanya watu wengi kukimbilia kufunga ndoa na majini - KULUNZI FIKRA

Friday, 27 October 2017

Tatizo linalofanya watu wengi kukimbilia kufunga ndoa na majini

 
 Akifanya mahojiano na kituo kimoja cha redio jijini Mombasa nchini Kenya, Tabibu wa Jadi kutoka nchini Tanzania, ajulikanae kama Mungwa Kabili almaarufu kama mungu wa kabili ameelezea sababu kwanini watu wengi siku hizi wanakimbilia kufunga ndoa na majini tofauti na ilivyo kuwa miaka ya nyuma ambapo watu walikuwa wananunua majini kwa ajili ya kushirikiana nayo katika mambo y mbalimbali.

“ Miaka ya nyuma , watu walio kuwa wanataka majini walikuwa wanakwenda kuwanunua moja kwa moja. Lakini siku hizi hali ni tofauti kidogo. Watu wanao taka msaada wa majini, hutumia njia ya kufunga nao ndoa. Hii ni kwa sababu njia hii inaonekana kuwa rahisi na yenye masharti nafuu ikilinganishwa na njia ya kuwanunua. “

Wimbi kubwa la watu wanao kimbilia kufunga ndoa na majini hufanya hivyo kwa sababu kuu zifuatazo ;

1. Kutafuta ulinzi binafsi wa fedha mali na mwili.. Hapa mfanya biashara mwenye mafanikio kwa kuhofia mali zake kupukutika kwa kuchezewa na wachawi au kufanyiwa hila na wabaya wake, huamua kuoa jini ili amsaidie kulinda mali na fedha zake.

2. Wengine hukimbilia kufunga ndoa na majini kwa sababu ya kutaka fedha , mali na utajiri : Hapa mtu anae tafuta mali na utajiri huchagua njia ya kufunga ndoa na jini anae weza kumsaidia utajiri . Jini huyu humsaidia muhusika kupata utajiri kwa njia ya kumvutia wateja kwenye biashara , kumkutanisha na watu wenye uwezo wa kumsaidia nakadhalika.

3. Wengine hufunga ndoa na majini kwa sababu ya kutafuta msaada katika kazi wanazo zifanya mfano, baadhi ya matabibu wa jadi na watabiri hufunga ndoa na majini wanao toka katika koo za kiganga ili wawasaidie katika kazi ya tiba. Wachimbaji madini, wafanyabiashara kadhalika

Kutafuta ulinzi, mali , fedha na utajiri, au kulinda mali, fedha na utajiri kwa njia ya kufunga ndoa na majini kunakimbiliwa na watu wengi kwa sababu masharti yake yanaonekana kuwa nafuu kuliko kutumia njia ya kununua majini moja kwa moja kwa sababu njia ya kununua majini moja kwa moja ina masharti mengi mazito na gharama za kuwatunza majini hao wa kununua ni kubwa sana.

Ndio maana watu wengi huamua kufunga ndoa na majini.

Hata hivyo suala la binadamu kufunga ndoa na majini halijaanza jana wala juzi na halitoweza kuisha kesho wala kesho kutwa.

Jambo hili limeanza tangu nyakati za Biblia. Mfano mzuri tunaupata kwa nabii Suleyman ambae miongoni mwa wake na masuria wake walikuwa majini na walikuwa na mchango mkubwa sana katika hekima na utajiri wake.

Akijibu swali kuhusu namna binadamu anavyo weza kufunga ndoa na jinni, Dokta Mungwa alisema “ Zipo njia nyingi sana zinazo tumika katika ndoa baina ya binadamu na jinni. Moja wapo kati ya njia zinazo tumika ni pamoja na hii ya kutumia MAFUTA YA MAJINI au MAFUTA YA BAHARINI …

Mtu anae taka kufunga ndoa na jini hutakiwa kuoga kwa dawa maalumu na kujifukiza mafusho maalumu. Baada ya hapo atatakiwa kukaa kwenye chumba cha peke yake kwa muda wa siku saba huku akila mara mbili kwa siku chakula cha kwanza anatakiwa kula saa moja usiku na mlo unao fuata atatakiwa kuula saa sita usiku.

Katika kipindi chote hicho hatakiwi kuongea wala kuwasiliana na mtu yoyote yule na atatakiwa kuwa anajipaka mafuta ya majini au mafuta ya baharini kila anapo maliza kula chakula.

Hayo mafuta ya majini au mafuta ya baharini anatakiwa kuwa anajipaka mwili mzima na akishamaliza kujipaka anakaa kwa muda wa robo saa anajikwangua mwili mzima ili kupata uchafu wa mwili wake ulio changamana na mafuta ya majini. Huu uchafu anakuwa ana uhifadhi kwenye chombo maalumu.

Baada ya siku saba, siku itakayo fuata atatakiwa kwenda baharini saa sita kamili mchana akiwa na huo uchafu alio jikwangua na ku uhifadhi kwa muda wa siku saba , mafuta ya baharini, pete mbili za baharini, kuku mweupe pamoja na vitu vingine vya kiganga ambavyo si lazima kuviweka wazi hapa redioni.

Akifika baharini atatakiwa kukaa baharini kuanzia saa sita kamili za mchana hadi saa saba kamili za usiku. Ikifika saa saba kamili za usiku atatakiwa kutoka ndani ya bahari na kufuata maelekezo mengine kuhusiana na hizo pete mbili za baharini, mafuta ya baharini na vitu vingine.

Akiwa ndani au nje ya bahari anaweza kukutana na vitu ambavyo hajawahi kuviona katika maisha yake ,lakini hatakiwi kuogopa kwa sababu hayo ndio maisha ambayo anakuwa ameyachagua.

Zipo njia nyingi sana lakini kwa leo nadhani njia hii inatosha.

Unapokuwa katika ndoa na jinni hakikisha unakuwa msafi sana na unafuata masharti yote atakayo kupa vinginevyo inavyo weza kukuletea madhara makubwa na mambo yanaweza kugeuka nje ndani.

Nilijaribu kutafuta namba anayo tumia Dokta Mungwa Kabili pindi awapo nchini Kenya lakini sikuweza kuipata.

No comments:

Post a Comment

Popular