Sumaye yashangazwa na wala rushwa wazidi kupandishwa vyeo - KULUNZI FIKRA

Sunday, 29 October 2017

Sumaye yashangazwa na wala rushwa wazidi kupandishwa vyeo

 
Waziri Mkuu Mstaafu Mhe  Fredrick Sumaye amelaani vikali watu waliomshambulia Rais wa chama cha sheria nchini TLS Mhe Tundu Lissu na kusema kamwe watu hao na wale waliowatuma hawatapata amani wala kufurahia maisha.

Akihutubia umati mkubwa wa watu wakati akimnadi mgombea udiwani wa Chadema Kata ya Mbweni Dar es salaam,Mhe Sumaye amewataka wakazi wa Mbweni kumpigia kura nyingi mgombea wa Chadema ili kuumgana na dunia kulaani kitendo alichofanyiwa Tundu Lissu.

Mhe Sumaye pia alishangazwa na hatua ya wala rushwa kupandishwa vyeo na kuonya hiyo ni aibu kubwa kwa CCM na serikali yake.

Mhe Sumaye ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chadema kanda ya Pwani na mjumbe wa Kamati Kuu amewataka wasimamizi wa uchaguzi huu kusimamia kwa haki vinginevyo kamwe Chadema haitakubali kuibiwa kura.

Mhe Sumaye ambaye alikuwa akishangiliwa kwa mayowe amesema kwa sasa Taifa liko katika hali mbaya kiuchumi na kusema CCM imeshindwa kutawala kwani maisha ya watu yamezidi kuwa magumu na kuonya Taifa linaelekea pabaya.

Maelfu ya watu waliohudhuria mkutano huo wameahidi kutoa kura nyingi kwa Chadema kiasi kwamba CCM wataona hata aibu kuiba kura.

No comments:

Post a Comment

Popular