Rais John Magufuli ni mgeni rasmi katika mkutano mkuu wa 33 wa kawaida wa Jumuia ya Tawala za Mitaa (ALAT).
Mwenyekiti wa ALAT, Gulamhafeez Mukadam amesema, awali mkutano huo ulipangwa kufanyika Septemba 19 hadi 22 lakini kutokana na baadhi ya wanachama kutokusanya fedha kwa wakati, umesogezwa na sasa utafanyika Oktoba 2 hadi 5 mkoani Mbeya.
Amesema kutokana na mamlaka za Serikali za mitaa kuwa wanachama wa Alat na Rais ndiye mwenye dhamana na Serikali za Mitaa, hivyo atakuwa mgeni rasmi katika mkutano huo.
Mkutano huo ni fursa ya kuwakutanisha viongozi wakuu wa Serikali Kuu na za mitaa kwa ajili ya kutoa maelekezo na miongozo ya kisera kwa watekelezaji ambao ni mamlaka ya serikali za mitaa nchini.
Mukadam amesema kuwa kauli mbiu ya mkutano huo ni “Ardhi kwenye mamlaka ya Serikali za Mitaa ni chachu ya maendeleo, halmashauri zitenge ardhi kwa ajili ya uwekezaji wa viwanda vidogovidogo na vikubwa".
Amsema," Tutatumia mkutano huu kujikita zaidi katika suala zima la uwekezaji katika viwanda kwa kuhakikisha halmashauri zinakuwa mstari wa mbele kuunga mkono juhudi za kuwa na Tanzania ya viwanda."
Mkutano mkuu ulitarajia kukutanisha wajumbe zaidi ya 400 kati yao wakiwa mameya 180 kutoka halmashauri zote nchini, wakurugenzi wa halmashauri wapatao 180, wawakilishi wa mikoa na wizara mbalimbali ambao jumla yao wanafika zaidi ya 400.
Tuesday, 3 October 2017
Home
Unlabelled
Rais Magufuli kuwa mgeni rasmi wa mkutano mkuu wa Jumuiya ya Tawala za mitaa (ALAT)
Rais Magufuli kuwa mgeni rasmi wa mkutano mkuu wa Jumuiya ya Tawala za mitaa (ALAT)
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Popular
-
THIS ANNOUNCEMENT CONTAINS INSIDE INFORMATION Acacia Mining plc (“Acacia” or the “Company” or the “Group”) Management Changes Ac...
-
Tanzania’s Tunduru district is a major producer of gem-quality sapphire and ruby, along with exotic gems such as alexandrite and tsavor...
-
Moto mkubwa umelipuka na kuunguza soko la wafanyabiashara wadogo wadogo (machinga) katika eneo la Mbagala Rangi Tatu – Dar, asubuhi hii M...
-
Ofisi ya Spika wa Bunge imesema, mpaka sasa haijapokea barua toka kwa aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Singida Kaskazini kupitia Chama cha...
-
Spika wa zamani, Pius Msekwa amesema Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu hakuwa analazimika kuandika barua kwa Spika wa Bunge...

No comments:
Post a Comment