Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli anatarajia kuwasili mkoani Mwanza oktoba 30 mwaka huu kwa ziara ya kikazi ambapo akiwa mkoani humo anatarajiwa kutembelea, kuzindua na kufungua miradi mbalimbali ya maendeleo.
Akizungumza na waandishi wa habari Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella amesema Rais Magufuli atawasili uwanja wa ndege wa Mwanza majira ya saa 2:30 asubuhi na kulakiwa na viongozi mbalimbali wa chama na serikali.
Amesema Rais Magufuli anatarajiwa kufanya ziara hiyo ya kikazi kwa siku mbili ambapo akiwa katika siku kwanza anatarajiwa kutembelea na kuzindua daraja la waenda kwa miguu lililopo eneo la Furahisha wilayani Ilemela ambapo ujenzi wake umekamilika, na kisha kufungua kiwanda cha vinywaji Baridi cha Sayona Drinks limited kilichopo Nyakato wilaya ya Nyamagana mjini humo.
Mongella amesema katika siku yake ya pili ya ziara hiyo, Rais Magufuli atafungua kiwanda cha Vifungashio cha Victoria Molders and Polybags kilichopo eneo la Igogo na baadaye atafungua kiwanda cha Dawa za binadamu cha Prince Pharmaceutical kilichopo Buhongwa wilaya ya Nyamagana.
Kutokana na ujio huo, Mkuu wa mkoa ametumia nafasi hiyo kuwataka wananchi wote wa mkoa wa Mwanza hasa maeneo ambayo Rais Magufuli atatembelea kujitokeza kwa wingi ambapo atatumia fursa hiyo kuzungumza na wananchi hao.

No comments:
Post a Comment