Rais Magufuli afanya mabadiliko makubwa katika baraza la mawaziri - KULUNZI FIKRA

Saturday, 7 October 2017

Rais Magufuli afanya mabadiliko makubwa katika baraza la mawaziri

 
 Rais Magufuli ametangaza mabadiliko katika Baraza la Mawaziri na pia kuteua Katibu mpya wa Bunge.

Wizara zimeongezeka kutoka 19 hadi 21, Mawaziri kutoka 19 hadi 21, Manaibu Waziri kutoka 16 hadi 21.

Rais Magufuli: Pia tumeongeza Mawaziri 2 na Manaibu Waziri 5

Rais Magufuli: Waziri wa Mazingira amebaki kuwa January Makamba, Naibu atakuwa Mh. Kangi Lugola"

Rais Magufuli: Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi tumeigawa na kuwa Wizara 2 za Wizara ya Kilimo na Wizara ya Mifugo na Uvuvi

Selemani Jaffo amepandishwa na kuwa Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI, kabla alikuwa Naibu kwenye Wizara hiyo.

Mbunge George Mkuchika ameteuliwa kuwa Waziri Ofisi ya Rais Utawala Bora.

Rais Magufuli: Mbunge Luhaga Mpina ameteuliwa kuwa Waziri wa Mifugo na Uvuvi na Abdallah Ulega ameteuliwa kuwa Naibu Waziri katika Wizara hiyo.

Wizara ya Fedha na Mipango itaendelea kuwa chini ya Waiziri Dr Philip Mpango na Naibu Waziri Dr Ashatu Kijaji

Wizara ya Kilimo Waziri ni Charles John Tzeba, na Naibu Waziri ni Marry Mwanjelwa

Wizara ya Habari utamaduni wasanii na Michezo, Waziri ni Harrison Mwakyembe na Naibu Waziri ni Juliana Shonza

Wizara ya Madini, Waziri ni Angela Kairuki na Naibu Waziri Harun S Nyongo

Wizara ya Nishati, Waziri atakuwa Medadi Kalemani Naibu Waziri atakuwa Subira Hamisi

Katibu wa bunge Steven Kagaigai na Dkt. Thomas Kashilila atapangiwa kazi nyingine

No comments:

Post a Comment

Popular